Andre Villas-Boas ameripotiwa kuwemo katika orodha fupi ya mameneja ambao watachukua nafasi ya bosi wa sasa aliye ‘under-pressure’ wa klabu ya Barcelona Tata Martino.
Inaweza ikawa ni kichekesho kufikiri kuwa meneja huyo ambaye ni karibuni tu aliifanya Manchester City ya England kama timu ya ridhaa lakini akiwekwa katika mazingira hatari ya kukosa kazi.
Na jimbo la kustaajabisha kuwa Barca wanamfikiria mtu kama Villas-Boas ambaye kimsingi alishindwa kazi na alikuwa katika wakati mgumu wakati huo katika vilabu vya England vya Tottenham na Chelsea.
Katika hatua nyingine habari kutoka katika magazeti ya jiji la Barcelona zinaarifu kuwa Villas-Boas anatajwa kuwa ni miongoni mwa watu watano ambao wanaweza kuchukua nafasi hiyo endapo Martino atatimuliwa kazi.
Licha ya kuwa katika mazingira ya kusonga mbele katika michuano ya Champions League, bado wanaburuzwa na Real Madrid wakiwa nyuma kwa alama tatu katika ligi maarufu ya Hispania La Liga. Vipigo viwili mwezi huu kutoka kwa Valencia na Real Sociedad Jumamosi ni vipigo ambavyo vimeichanganya bodi ya Barca.
Meneja Tata Martino aliye katika kipindi kigumu Barcelona |
Villas-Boas, kocha wa Celta Vigo Luis Enrique na bosi wa Athletic Bilbao, Ernesto Valverde wanawekwa katika nafasi ya kurithi nafasi hiyo ambao wanaonekana kuziba nafasi vizuri kulingana na filosofia ya klabu hiyo.
Pia wapo Diego Simeone wa Atletico Madrid na bosi wa Borussia Dortmund Jurgen Klopp.
No comments:
Post a Comment