Wakati
Zambia (Shepolopolo) imewasili leo mchana (Februari 27 mwaka huu), Twiga Stars
imesema mazoezi yamewaingia barabara tayari kwa mechi dhidi ya Wazambia hao
itakayochezwa kesho (Februari 28 mwaka huu).
Mechi
hiyo ya marudiano ya raundi ya kwanza ya michuano ya Afrika kwa Wanawake (AWC)
itafanyika Uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi kuanzia saa 10 kamili jioni,
na hakutakuwa na kiingilio.
Wakizungumzia
mechi hiyo, Kocha wa Twiga Stars, Rogasian Kaijage na nahodha wa timu hiyo
Sophia Mwasikili wamesema kikosi chao kimewiva kwa ajili ya mpambano huo baada
ya kufanyia kazi upungufu uliojitokeza katika mechi ya kwanza.
Twiga
Stars ilipoteza mechi ya kwanza iliyochezwa Februari 14 mwaka huu jijini Lusaka
kwa mabao 2-1, na inahitaji ushindi ili iweze kusonga mbele kwenye michuano
hiyo ambayo fainali zake zitafanyika Oktoba mwaka huu nchini Namibia.
Iwapo
Twiga Stars itafanikiwa kuitoa Zambia katika mechi hiyo itakayooneshwa moja kwa
moja na Azam Tv itacheza raundi ya mwisho na Zimbabwe.
Msafara
wa Shepolopolo una watu 26 ambapo wachezaji ni Anita Mulenga, Annie Kibanji, Carol
Howes, Debora Chisanga, Emelda Musonda, Esther Mukwasa, Grace Zulu, Hazel Nali,
Hellen Mubanga, Lweendo Chisamu, Meya Banda, Mirriam Katamanda, Misozi Zulu, Mupopo
Kabange, Noria Sosala, Rachel Lungu na Susan Banda.
Viongozi
ni Maclean Daka, Charles Bwale, Kaluba Kangwa, Enala Phiri, Cornelia Chazura,
James Nyimbili, Besa Chibwe, Dorothy Sampan a Kabungo Katongo
No comments:
Post a Comment