Mchezaji maarufu wa tennis wa Uingereza, Andy Murray amefuzu
kucheza hatua ya robo fainali ya michuano ya wazi ya Mexico baada ya kumtoa
Joao Sousa wa Ureno kwa seti 6-3 6-4 katika viwanja vya tenis huko Acapulco.
Murray anayeshika nafasi ya pili kwa viwango vya ubora wa
tennis duninai, anatafuta kucheza nusu fainali yake ya kwanza mwaka huu,
atakapopambana na Gilles Simon wa Ufaransa.
David Ferrer naye alimcharaza Mhispania mwenzake Feliciano
Lopez kwa seti 7-6 (7-1) 6-2.
Grigor Dimitrov wa nne kwa ubora alimng'oa Marcos Baghdatis
katika hatua ya robo fainali kwa seti 6-1 6-4 na atapambana na Ernests Gulbis,
wa saba katika ubora wa viwango vya tennis ambaye alimfunga David Goffin kwa
seti 6-1 3-6 7-6 (7-5).
Murray, ambaye ambaye alikuwa katika kundi moja na Dimotrov
na Gulbis, alianza taratibu alipovaana na Sousa - kama alivyofanya katika
mzunguko wa kwanza walipokutana na Pablo Andujar.
Bingwa huyo wa Wimbledon aliweza kumtisha Sousa kutokana na
upigaji wa mipira na kumlazimisha mchezaji huyo anayeshikilia nafasi ya 44 kwa
ubora kuzidi kufanya makosa kutokana na shinikizo alilokuwa akipata kutoka kwa
Murray.
Murray sasa atakabiliana na Simon, anayeshika nafasi ya 23,
Ijumaa. Mwingereza huyo anajivunia ushindi wa 11-1 dhidi ya Simon katika
michezo waliyopambana awali.
No comments:
Post a Comment