Timu inayoongoza Ligi ya Premia itakutana na inayoshika mkia Jumamosi
pale itakapo safiri kuifuata Fulham wakijaribu kuweka salama jitihada zao za kupigania taji na kuongeza masaibu ya majirani hao wanaokabiliwa na
hatari ya kushushwa daraja.
Huku Manchester City walio katika nafasi ya tatu wakitarajiwa kukutana dhidi ya Sunderland
katika fainali ya Kombe la Capital One (League) uwanjani Wembley
Jumapili.
Chelsea wanaweza kuongeza mwanya kati yao na vijana hao wa
Manuel Pellegrini hadi alama sita.
Chelsea wanaongoza wakiwa na alama 60 baada ya kushuka uwanjani katika michezo 27, moja zaidi ya
Arsenal yenye alama 59, ambao watakuwa ugenini kwa Stoke Jumapili, na wako alama
tatu mbele ya City, wenye alama 57 kutoka kwa mechi 26.
Liverpool
wako nambari nne na alama 56.
Timu hiyo ya Jose Mourinho ilishindwa mara ya mwisho na Fulham 2006,
mwaka ambao walishinda taji lao la pili mtawalia, na walitoka sare ya
1-1 na Galatasaray katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano.
"Sharti tupambane, lazima tucheze. Kila ushindi utaendelea kutuweka
huko, kila kichapo au sare ina maana kwamba tutapoteza nafasi yetu.”
Fulham, ambao hawajashinda kwa mechi saba sasa, watakuwa wakitarajia
kumpa kocha wao mpya kutoka Ujerumani Felix Magath ushindi katika mechi
yake ya pili baada ya kutoka sare dhidi ya West Bromwich
Albion wikendi iliyopita.
Arsenal walio wapili, na waliolaza Sunderland 4-1 mechi yao
iliyopita, wataenda Stoke wakiwa wametatizika kupata ushindi uwanja wa
Britannia.
Arsene Wenger hajaweza kushinda Stoke katika mechi tatu zilizopita
akiwa kwao na Mfaransa huyo atakuwa bila beki wa kushoto Kieran Gibbs
ambaye anauguza jeraha la misuli ya paja.
“Bado tuko hapo kwenye jedwali,” Wenger alisema baada ya ushindi
dhidi ya Sunderland. "Yote yatategemea uendelevu wa matokeo yetu.”
Stoke, ambao wameshinda mechi moja pekee kati ya sita za ligi
walizocheza majuzi, wako alama tatu kutoka kwa eneo la kushushwa ngazi
lakini watatiwa nguvu na kurudi kwa difenda Mjerumani Robert Huth.
Liverpool wataendelea kutishia viongozi watatu wa ligi watakaposafiri
pwani ya kusini kucheza dhidi ya Southampton Jumamosi (1730), straika
wao Daniel Sturridge akilenga kufunga katika mechi yake ya tisa
mfululizo Ligi ya Premia.
No comments:
Post a Comment