Mlinzi wa Atalanta
Federico Peluso amefanyiwa vipimo vya afya hii leo katika klabu ya Juventus na
anatarajiwa kukamilisha taratibu za usajili wake hii leo
Mpango wa
uhamisho wake ni wa gharama ya euro milioni 1.5 ambapo Bianconeri(Juve) wakiwa
na maamuzi ya uhamisho wa kudumu baada ya msimu kumalizika.
Endapo klanbu
hiyo itachagua kufanya hivyo, inamaanisha kuwa mabingwa hao wa kandanda nchini
Italia watalazimika kulipa eoro milioni 3.5 kwa kupata huduma yake na huku
mlinzi huyo wa kati akitarajiwa kuongeza ushindani katika sehemu ya ulinzi wa
kati na ulinzi wa kushoto
Taarifa ya
klabu kupitia mtandao wake imethibitisha kuwa mchezaji huyo atafanyiwa vipimo
hivyo kule Turin kunako taasisi ya tiba za michezo
Peluso alijiunga
Atalanta mwaka 2009 akitokea AlbinoLeffe na amekwisha itumikia timu ya taifa ya
Italia michezo mitatu.
Ronaldo: Nadhani
Mourinho atasalia.
Cristiano
Ronaldo anaamini kuwa kocha wake Jose Mourinho atasalia katika klabu yake ya Real
Madrid.
Mreno huyo
ameanza kuona hatma yake katika klabu hiyo kama inamashaka hasa kutoka na gumzo
lililoanza kuchomoza hususani kutokana na Madrid kuachwa kwa mbali na mahasimu wao wa soka la Hispania Barcelona kwa tofauti ya
alama 16 katika msimamo wa ligi ya Hispania La Liga.
Hata hivyo,
Ronaldo haoni kwamba hiyo ndiyo inaweza kuwa sababu ya kumuondosha Mourinho Santiago
Bernabeu, na kusisitiza kuwa bado ni mtu sahihi wa kuendelea kuiongoza klabu
hiyo.
Akinukuliwa na
vyombo vya habari baada ya kuulizwa juu ya uwezekanao wa Mourinho kuondoka
Ronaldo alijibu
"Sijui,
itategenea na hali ya mambo itakavyokuwa ndani ya klabu, kwa upande wangu ningependa
asalie kwakuwa ni kocha sahihi. Ni kocha wa kiwango cha juu katika timu ya
kiwango cha juu. Nadhani atasalia lakini kila mtu ana uchaguzi wake wa mambo
yake ya baadaye"
Mourinho alianza
kuingia matatizoni kuanzia pale alipoamua kumuweka benchi mlinda mlango namba
moja Iker Casillas na kupelekea kichapo kutoka kwa Malaga, lakini Ronaldo anasema
maamuzi ya kocha ni ya mwisho.
WAKALA: Pato
anaelekea kukamilisha uhamisho wake Corinthians.
Mshambuliaji
wa AC Milan Alexandre Pato anakaribia kukamilisha taratibu za uhamisho wake
kuelekea Corinthians, hii ni kwa mujibu wa wakala wa mchezaji huyo Gilmar
Veloz.
Kipindi cha
utumishi wake wa miaka 23 katika viunga vya San Siro ulitiwa doa na majeraha
ambapo taarifa zinasema sasa ameamua kurejea katika ardhi ya nyumbani.
Kuna vilabu
kadhaa barani ulaya vimekuwa katika mawindo ya kumtaka Pato, lakini mwakilishi
wake amesisitiza kuwa Pato atarejea nyumbani Brazil hivi karibuni.
Benitez:
Torres yuko tayari kuwekwa benchi falcao anakuja.
Kocha wa
muda wa Chelsea Rafael Benitez, amesisitiza kuwa Fernando Torres atamuelewa tu endapoa atalamika kumuweka benchi katika baadhi ya michezo, wakati huu ambapo klabu hiyo inataka
kusajili vijana zaidi katika safu yake ya ushambuliaji katika kipindi hiki cha
dirisha dogo la usajili.
Mshambuliaji
huyo wa kimataifa wa Hispania alikuwa akihangaika katika kipindi kirefu kusaka
kurejesha kiwango chake tangu
aliposajiliwa kutoka Liverpool januari 2012 ambapo angalau kiwango hicho
kimeongezeka mara baada ya kuwasili kwa Bernitez.
Mwezi wa November,
klabu hiyo kutoka kaskazini mwa jiji la London ilikuwa katika mazungumzo na
mshambuliaji wa Atletico Madrid Radamel Falcao ambapo Benitez anaamini kuwa
mchezaji huyo ataleta ushinda wenye afya zaidi katika safu yake ya
ushambuliaji.
No comments:
Post a Comment