Bondi
wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali anatarajiwa kupanda ulingoni
Januari 12 katika ukumbi wa Friends Corner Manzese Jijini Dar es Salaam
kutetea Ubingwa wa Afika Mashariki.
Akiongea
na waandishi wa habari Mratibu wa pambano hilo Aisha mbegu alisema
mashali atapambana kuzipiga na Mkenya Bernard Mackoliech mpambano
utakaokuwa wa raundi 10.
Alisema
maandalizi yamekamilika ikiwa pia na kutumiwa tiketi kwa bondia huyo
mkenya ambaye anatarajiwa kuwasili januari nane kwa ajili ya kupima
uzito na kupanda ulingoni.
“tunataraji
mpambano utakuwa mkali wa kukata na shoka ukizingatia mashali ameweka
kambi kwa muda mrefu nje ya mkoa lakini pia Mackoliech ni bondia mahiri
ambaye anasaka rekodi ya kwenda kucheza nje ya nchi”,alisema Aisha.
Alisema
nafasi iko wazi kwa watu wanaotaka kudhamini ili kuhakikisha mpambano
huo unafanikiwa ukizingatia ndio mpambano wa kwanza kwa mwaka 2013 na
pia mashali anavutia mashabiki wengi.
Kwa
upande wake rais wa TPBO amesema mapambano ya utangulizi yanatarajiwa
kuwa manne na mabondi tayari wamesaini mikataba na watatangazwa hivi
karibuni.
Bondia
Thomas Mashali anatetea ubingwa huo wa Afrika mashariki na kati ambao
aliupata baada ya kumpiga Mganda Medi Sebyala Jijini Dar es salaam
mpambano uliohudhuriwa na mashabiki lukuki.
No comments:
Post a Comment