KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, October 12, 2013

Ujerumani, Ubelgiji, na Uswisi zatua Brazil na kupelelea mataifa 13 mpaka sasa kukata tiketi ya kombe la dunia.

Mesut Özil (kulia) aking'ang'ania mpira na mchezaji wa Ireland Simon Cox Mesut Özil (kulia) aking'ang'ania mpira na mchezaji wa Ireland Simon Cox

Ujerumani, Ubelgiji na Uswisi zimejikatia tiketi za kuingia katika fainali ya kombe la Dunia nchini Brazil, wakati Uhispania, England na Urusi pia zikishinda mechi zao hapo jana katika kuweka mazingira mazuri ya kutinga hatua hiyo muhimu kisoka duniani.

Kinyang'anyiro cha mwaka ujao, pia kinaonekana kukaribiwa na Bosnia-Herzegovina, ambayo haijawahi kucheza katika Kombe la Dunia, lakini Christiano Ronaldo anaonekana kuingia katika duru ya mchujo pamoja na timu yake ya Ureno, baada ya usiku ambao picha kamili ya kufuzu katika makundi yote 9 ilijitokeza wazi.

Uholanzi ambayo tayari ilikuwa imejikatia tiketi ya Kombe la Dunia kabla ya kuichabanga Hungary mabao manane kwa moja, ikiwa ni pamoja na mabao matatu kutoka kwa Robin van Persie ambayo yalimweka mshambuliaji huyo wa Manchester United juu ya chati ya mfungaji wa mabao mengi nchini mwake, akiwa na 41.
Marouane Fellaini wa Ubelgiji (Kulia) akipambana na Mcroatia Ivan Strinic (Kushoto) na Mateo Kovacic (Katikati) Marouane Fellaini wa Ubelgiji (Kulia) akipambana na Mcroatia Ivan Strinic (Kushoto) na Mateo Kovacic (Katikati)

Ujerumani ilipata ushindi rahisi wa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Jamhuri ya Ireland, kupitia mabao ya Sami Khedira, Andre Schuerrle na Mesut Özil, na kujihakikishia nafasi ya kwanza katika kundi C, na kufika katika tamasha hilo maarufu la soka kwa mara ya 16 mfululizo.

Kwa Ubelgiji, hata hivyo, itakuwa mara yao ya kwanza katika Kombe la Dunia baada ya miaka 12 kufuatia kile kinachofahamika kama kizazi kipya cha nchi hiyo kuongoza kundi A kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja dhidi ya Croatia, huku Romelu Lukaku akitikisa wavu mara mbili.

 Uswisi iliishinda Albania mabao mawili kwa moja na kuongoza kundi E na kujihakikishia nafasi nchini Brazil wakati kumesalia mechi moja.

 Uhispania ilitoka jasho jembamba licha ya kufanikiwa kuibwaga Belarus magoli mawili kwa moja kupitia Xavi Hernandez na Alvaro Negredo katika kipindi cha pili, na sasa inahitaji alama  moja tu katika mchezo wa nyumbani itakapocheza na Georgia ili kujihakikishia nafasi ya kulitetea kombe hilo mwaka ujao.

England iliendelea kuongoza kundi H, ikiwa na pengo la alama moja mbele ya Ukraine, baada ya kuonyesha mchezo mzuri katika kipindi cha pili ambapo iliishinda Montenegro mabao manne kwa moja, huku washambuliaji Wayne Rooney na Daniel Sturridge pamoja na Andros Townsend ambaye alipewa fursa ya kuichezea timu ya taifa kwa mara ya kwanza, wakiwa wafungaji.
Wabelgiji wamesheherekea usiku kucha kufuatia kufuzu timu yao ya taifa katika dimba la dunia Wabelgiji wamesheherekea usiku kucha kufuatia kufuzu timu yao ya taifa katika dimba la dunia.
 
Vijana hao wa kocha Roy Hodgson wanahitaji ushindi dhidi ya Poland Jumanne wiki ijayo na kufuzu moja kwa moja, lakini wakitoka sare, watawapa nafasi Ukraine ambao waliwabwaga Poland bao moja kwa nunge, na wanamchezo rahisi uliosalia dhidi ya San Marino.

 Urusi waliwazaba Luxembourg mabao manne kwa sifuri na sasa wako mbele ya Ureno kwa tofauti ya alama tatu huku wakihitaji sare tu dhidi ya Azerbaijan ili kujihakikishia nafasi ya kwanza.

 Ureno iliyofungwa goli zikisalia dakika tano mchezo kuisha na kupelekea kutoka sare ya goli moja kwa moja dhidi ya Israel.

 Ugiriki iliichapa Slovakia bao moja kwa sifuri na wako alama sawa na Bosnia ijapokuwa inazidiwa kwa  tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

 Kwingineko, Sweden imejiunga na Croatia katika mechi za mchujo, baada ya kumaliza wa pili nyuma ya Ujerumani kwa kuwashinda Austria magoli mawili kwa moja huku Zlatan Ibrahimovic akifunga bao la ushindi.

Italia ambayo ilifuzu pamoja na Uholanzi mwezi uliopita, ilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili na Denmark na kuwaacha Bulgaria katika nafasi ya pili kwa tofauti ya mabao katika kundi B, licha ya kichapo cha mabao mawili kwa moja kutoka kwa Armenia.

 Iceland imesalia nyuma ya Uswisi baada ya kuizidi nguvu Cyprus mabao mawili mtungi, wakati Uturuki na Romania zikishinda mechi zao matokeo yaliyowapa alama sawa nyuma ya Uholanzi huku kukiwa na mchezo mmoja uliosalia.

 Kwa ujumla, nafasi 13 kati ya nafasi 32 za Kombe la Dunia sasa zimejulikana. Marekani, Argentina, Australia, Costa Rica, Iran, Japan na Korea Kusini zilikuwa tayari zimejikatia tikiti, wakati Brazil ikipata kibali cha moja kwa moja kama mwenyeji wa dimba hilo.

No comments:

Post a Comment