KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, March 15, 2013

UPASUAJI WA LADSLAUSI MBOGO KATIKA PICHA (KUTOKA WWW.SAHEHJEMBE.BLOGSPOT.COM)

EXCLUSIVE: A TO Z YA UPASUAJI WA MBOGO, KUANZIA CHUMBA CHA UPASUAJI

Upasuaji wa beki wa Yanga, Ladslaus Mbogo umekuwa gumzo. Beki huyo wamepasuliwa uvimbe mkubwa uliokuwa kwenye shavu lake.
Upasuaji huo ulifanyika kwenye hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam, jana na kuongozwa na Daktari wa Yanga, Nassor Matuzya.
Baadaye wachezaji na viongozi walikwenda kumjulia hali Mbogo ambaye alionekana kuwa na hali nzuri na mwisho kuanza utani na wenzake. Beki huyo kajiunga na Yanga msimu huu akitokea Toto African ya Mwanza.
Mchezaji huyo anajulikana kwa jina la Mnyama na hivi karibuni aliingia katika rekodi ya kupiga daruga hadi kuchana kiatu cha mshambuliaji wa Yanga, Jerry Tegete.

Salehjembe inakuletea picha kutoka ndani ya chumba cha upasuaji, hadi dakika chache kabla ya shughuli hiyo kuanza. Mwenyezi Mungu amsaidie Mbogo apone haraka na kurejea uwanjani aendelee na majukumu yake.
 Kabla upasuaji haujaanza...
Tayari kwa kuanza upasuaji...

No comments:

Post a Comment