KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, March 16, 2013

LIGI DARAJA LA KWANZA(FDL) GREEN WORRIORS NA POLISI KUMALIZA MSIMU KARUME. ASHANTI NA MORO UNITED KIVUMBI KESHO.

Kikosi cha Ashanti kilichorejea ligi kuu.
Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2012/2013 unamalizika wikiendi hii huku timu za Mbeya City ya Mbeya, Ashanti United ya Dar es Salaam na Rhino Rangers ya Tabora zikiwa tayari zimepata tiketi ya kucheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu ujao.
 
Leo jioni (Machi 16 ) katika kundi B kutakuwa na mchezo baina ya Green Warriors vs Polisi Dar (Karume, Dar es Salaam) na Ndanda vs Villa Squad (Nangwanda Sijaona, Mtwara). 
Katika kundi C hii leo (Machi 16 ) Polisi Tabora vs Pamba (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

Kundi A mechi zote zitachezwa Jumapili (Machi 17 mwaka huu) ambapo Majimaji vs Mbeya City kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea, Kurugenzi vs Mkamba Rangers (Mafinga) na Burkina Faso vs JKT Mlale (Jamhuri, Morogoro).

 Keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) ni Moro United vs Ashanti United (Karume, Dar es Salaam) na Tranist Camp vs Tessema (Mabatini, Mlandizi). 

Keshokutwa (Machi 17 mwaka huu) ni Polisi Mara vs JKT Kanembwa (Karume, Musoma), Polisi Dodoma vs Mwadui (Jamhuri, Dodoma) na Rhino Rangers vs Morani (Ali Hassan Mwinyi, Tabora).

No comments:

Post a Comment