Bosi wa Chelsea Rafael Benitez amethibtisha
kuwakosa Cahill na Ashley Cole ambao wanasumbuliwa kuelekea kwenye michezo
ijayo.
Cole aliumia hii leo wakati
akimkimbiza Danny Wellbeck na kutolewa nje ya uwanja katika mchezo wa kwanza wa
michuano ya FA dhidi ya Manchester United mchezo ambao Chelsea iliibuka na
ushindi wa goli 1-0.
Kwa upande wake Cahill, ambaye
aliondolewa katika kikosi cha England kilichokuwa katika kampeni ya kufuzu
kombe la dunia lakini vilevile hakuwepo
katika kikosi cha Chelsea kilichochapwa bao 2-1 na Southampton.
Alipoulizwa kuhusina na hali ya Cole,
Benitez amesema
"aina hii yamaumivu ina maana
atakosekana si chini ya wiki mbili, inaweza kuwa hata michezo au kitu kama
hicho''
Cahill inawezekana akakosekana kwa
siku 15.
Hiyo ina maanisha kuwa Cahill na Cole
watakosekana kwa michezo yote ya robo fainali ya Europa League dhidi ya Rubin
Kazan pamoja na mchezo wa nyumbani wa ligi dhidi ya Sunderland.
Wote kuna wasiwasi wa kutokuwepo
katika nusu fainali ya FA dhidi ya Manchester City April 14.
Bayern Munich wanasema licha ya Juventus kuwa wagumu lakini mwendo mdundo.
Wachezaji wa Bayern Munich na maafisa
wa klabu hiyo wamesema ushindi wa kishindo wa mabao 9-2 katika ligi kuu ya soka nchini
Ujerumani Bundesliga dhidi ya Hamburg kamwe hauwafanyi kubweteka hata kidogo na
kwamba hiyo ni nguvu ambayo itaelekezwa katika mchezo Juventus hapo kesho.
Bayern inaongoza ligi kuu ya soka
nchini humo ikiwa mbele kwa alama 20 dhidi ya Borussia Dortmund na inaelekea
kushinda taji la Bundesliga ikiwa itashinda dhidi ya Eintracht Frankfurt wiki
ijayo lakini Jupp Heynckes anafikira zaidi Champions League.
"hatuutazami sana mchezo huo
tulipata ushindi mkubwa kwakuwa tunakabiliwa na mchezo mgumu Jumanne"
Winga wa klabu Thomas Muller, ambaye
alikuwa benchi kabla ya kuingizwa kunako dakika ya 64 anaamini kuwa mchezo
dhidi ya Juve utakuwa mgumu "
Amesema kuwa Juventus wanategemea
zaidi umoja na na kucheza kitimu zaidi na kwamba ukikutana na timu inayocheza
mchezo kwa njia hiyo mchezo huwa mgumu na kwamba inabidi wasahau ushindi wa huo
wa 9-2."
Mario Mandzukic pia alipumzishwa na Heynckes
alimuanzisha nyota wa kimataifa wa Peru Claudio Pizarro, ambaye alilipa fadhila
kwa kufunga magoli manne katika mchezo wa ushindi wa magoli 9-2.
Kiungo Bastian Schweinsteiger, ambaye
alistua maumivu ya kifungo cha mguu wake katika dakika za mwisho za mchezo
dhidi ya Hamburg anatarajiwa kuwa fiti na kuwepo dimbani katika mchezo dhidi ya
Juve.
Vilanova anajipanga kurejea kibaruani hii leo dhidi ya PSG.
Tito Vilanova sasa anajipanga kurejea
katika benchi la klabu yake ya Barcelona ‘blaugrana’
kwa mara ya kwanza tangu mwezi Januari huku Xavi Hernandez na Jodi Alba wakielekea
kurejea katika uimara wao kiafya baada ya kusumbuliwa na misuli.
Katika safari yao asubuhi ya jana Messi,
aliwaambia mashabiki kupitia mtandao wake wa Tencent Weibo kuwa yeye na
kikosi kizima cha klabu hiyo wamejipanga kukabiliana na kikosi cha mmiliki raia
wa Qatari ambao wanaongoza ligi Ligue PSG.
Amsema mchezo utakuwa mgumu lakini
wanajisikia safi kiushindani.
Kauli ya Messi kupitia mtandao wa
kijamii ni majibu ya wasiwasi uliotokana na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Celta
Vigo mchezo ambao Messi alifunga goli katika michezo 19 aliyofunga mfululizo
katika ligi kuu ya nchini Hispania La Liga.
Katika mchezo huo wa Jumamosi huko Balaidos
kiwango cha mshambuliaji Cristian Tello kilikuwa juu ambapo alifunga goli la
kwanza la Barca na kutengeza bao la pili lililofungwa na Messi.
Wakati Vilanova akiendelea kubembeleza hali ya afya
yake kurejea vema baada ya miezi miwili ya kuendelea na matibabu jijini New
York, msaidizi wake Jordi Roura alitarajiwa jioni ya jana kufanya mkutano na
waandishi wa habari kabla ya mazoezi huko Parc des Princes.
Mazoezi ya jana ya Barca yalitumika kumsaidia kocha kuunda kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo wa leo Jumanne.
Huenda Xavi akirejea katika kiungo na
Cesc Fabregas na Thiago Alcantara wanaendelea kusalia katika benchi sambamba na
Gerard Deulofeu.
David Villa huenda akaanza akiwa na Messi
na Tello au Alexis Sanchez, ambaye hakuwa vizuri katika mchezo dhidi ya Celta Virgo
na kutolewa kipindi cha pili.
Jumla ya mashabiki 2,300 wa blaugrana
wanatazamiwa kushuhudia mchezo huo huko Parc des Princes wakijumuika na
takribani wakurugenzi 20 wa Catalans.
No comments:
Post a Comment