Habari za kimataifa michezo
Mlinzi wa Sunderland Titus Bramble amepatikana na hatia ya makosa mawili likiwemo la udhalilishaji wa kijinsia pamoja na kujisaidia haja ndogo hadharani.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 30 anatarajia kusomewa mashtaka yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Teeside novemba 10.
Nyota huyo anayekipiga katika ligi kuu ya kandanda nchini Uingereza alikamatwa Septemba 28 na Octoba 14 kutokana na kutoa lugha chafu.
Wakili wa Bramble amesema atapingana vikali kuhusika na tuhuma hizo.
Msemaji wa Sunderland AFC amekaririwa akisema
"Titus Bramble anafanya mazoezi binafsi kwa sasa na hatahusika katika kikosi cha kwanza na kwamba itasalia hivyo kupisha klabu kufanya uchunguzi wa tuhuma ."
Mr Bramble alianza kucheza soka katika klabu ya Ipswich, kabla ya kujiunga na Newcastle United kwa uhamisho wa ada ya pauni milioni 6.
Baadaye alijiunga na Wigan Athletic na kurejea kaskazini/mashariki katika klabu yake ya zamani ya Sunderland mwaka jana.
Kenny Dalglish anataka mzozo wa Luis Suarez na Patrice Evra kumalizika
Meneja wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish anataka mzozo wa wa nyota wawili Luis Suarez na Patrice Evra kumalizika .
Chama cha kandanda nchini Uingereza (FA) kinachunguza juu malalamiko ya mlinzi wa Manchester United Patrice Evra ya kwamba alinyanyapaliwa na mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez.
Kenny Dalglish amekaririwa akisema
"tunapaswa kulimaliza hilo haraka na kulitupilia mbali “.
"yoyote atakae patikana na makosa anapaswa kuadhibiwa."
Kumekuwepo na tuhuma kwa Evra kwenda kwa Suarez kuwa alimtolea lugha chafu katika mchezo ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 kati ya Liverpool dhidi ya Manchester United mchezo ulichezwa katika dimba la Anfield mapema mwezi huu.
Emmanuel Adebayor-Manchester City ilikuwa pasua kichwa
Emmanuel Adebayor ameendelea kusisitiza kuwa katika kipindi chote alichokuwa katika klabu ya Manchester City alikuwa katika kipindi kigumu kiasi kunanisha na msemo wa pasua kichwa na kusema katu hajutii kuihama klabu hiyo.
Adebayor alijiunga na Tottenham kwa mkopo wa muda mrefu mwezi August baada ya kugandishwa katika kikosi cha kocha Roberto Mancini na mipango ya kocha huyo tangu mwezi December mwaka jana.
Akizungumza na BBC Sport amekaririwa akisema
"nawatakia kila la kheri lakini unadhani nataraji kuwa sehemu ya ya klabu hiyo ? hapana.
"kila nilipokuwa nikiamka kwenda katika mazoezi ya klabu ile nilikuwa najihisi kichwa kuuma."
Kikosi kipya kilicho kusanywa au kuundwa na kocha Mancini kwasasa kipo katika kilele cha ligi kuu ya Uingereza bila ya mshambuliaji huyo lakini hata hivyo mshambulioaji huyo wa zamani wa Arsenal striker anasema hajihisi kukosa kitu kwa kutokuwa na City baada ya kufanikiwa kujijengea mazingira huko London ya kaskazini.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Togo ameendelewa kukaririwa akisema
"kila mtu atataka kuwepo katika nyumba anayojisikia faraja,".
Mataifa mbalimbali barani Afrika yanasubiri kwa hamu Draw ya mataifa ya Afrika 2012
Jumla ya mataifa 16 hapo kesho jumamosi yatakuwa katika wakati muafaka kufanya tathmini na kujua wapinzani wao katika fainali ya soka ya mataifa ya Afrika pale ambapo Draw kubwa itakapo fanyika kuelekea katika fainali hizo.
Sherehe ya draw itafanyika jioni katika jiji la Malabo,mji mkuu mwenza wa wenyeji wa fainali hizo Equatorial Guinea
Mshangao mkubwa utaonekana hapo kesho miongoni mwa timu hizo 16 pale ambapo vyungu vinne vya glass vitakapo jumuisha timu za mataifa manne ambayo yatakuwa yakishiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza mataifa hayo ni Botswana, Niger na wenyeji wenza Equatorial Guinea.
Lakini hata hivyo itashudia pia mataifa kadhaa nguli katika soka la Afrika kutokuwemo katika vyungu hivyo baada ya kushindwa kufuzu katika hatua ya kufuzu kwa fainali hizo mataifa hayo ni Algeria, Cameroon, Egypt, Nigeria na Afrika Kusini.
Niger imefanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza pamoja na Equatorial Guinea ambao wanatumia faida ya uwenyeji wao.
Timu kiongozi katika chungu atakuwa ametegemea na uwezo wao katika michuano mitatu iliyopita na mkazo mkubwa ukiwa ni katika michuano ya hivi karibuni .
Equatorial Guinea pamoja na Gabon watakuwa timu kiongozi katika chungu cha kwanza pamoja na mabingwa mara nne wa michuano hiyo Ghana na mabingwa wa mwaka 1992 Tembo wa Ivory Coast.
Chungu namba mbili kutakuwa na timu za mataifa ya Angola, Guinea, Tunisia na Zambia wakati ambapo katika chungu cha tatu kutakuwa na mataifa ya Burkina Faso, Mali, Morocco na Senegal..
Chungu cha nne kitakuwa na mataifa ya Botswana, Libya, Niger na Sudan
Pele
mchezaji aliyefanikiwa kucheza kwa ushindi mara tatu Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya Brazil Abeid Pele anayejulikana na wengi kama ni mchezaji bora wa wakati wote amefanya uchaguzi wake juu ya mrithi wa mafanikio yake katika kipindi chote “personal greatest of all time”.
Hata hivyo haamini kama kuna mtu aliyecheza tangu kwa kiwango chake tangu alipoachana na mchezo huo ambaye anaweza kuvaa taji lake huku kwa muono wake akijitazama kama bado ni namba moja akiwa na umri wa miaka 71.
Anaamini hivyo na hadhani kama kuna watu wengi wanaotofautiana na mawazo yake.
Wengi wanasema Lionel Messi amevuka kiwango cha Diego Maradona, huku maoni ya Ossie Ardiles, akimnyooshea kidole Messi kuwa amefikia hadhi ya kuwa mchezaji bora wa muda wote .
Alipoulizwa na ESPN soccernet juu ya swali hilo Pelle ajibu hivi
"nadhani pele mwingine bado kuna ugumu kidogo kwasababu mama yangu na baba yangu walifunga yaani uzazi
"siku zote kuna wachezaji bora . pengine siku moja watatokezea wachezaji watakao cheza michezo mingi kuliko Pele hata kufunga magoli mengi kuliko Pele lakini nadhani hilo ni gumu ."
Pele amemtaja Messi kama ndiye mchezaji bora katika kizazi hiki ingawa bado anamtazama Neymar,kutoka katika klabu yake ya zamani ya Santos akamzidi mchezaji huyo nyota wa Barcelona.
Pele alitoa orodha yake ya nyota aliowaona katika vipindi tofauti tofauti ambao ni
"Beckenbaurer, Georgie Best, Zico, na Maradona,Platini,Di Stefano. Zidane. Wakati Fulani alifananishwa na Garrincha na Zico lakini leo kuna Messi na Neymar."
Amesema pia anafurahishwa na Wayne Rooney na Steven Gerrard.
No comments:
Post a Comment