KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Sunday, November 18, 2012

CHAMA CHA MCHEZO WA PETE (NETBALL) MKOA WA DAR ES SALAAM CHATAMBULISHA VIONGOZI WAKE.

Afisa Michezo Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii akiongea na wachezaji wa netiboli jana kwenye viwanja vya harbours view Kurasini
Baadhi ya viongozi wapya wa CHANEDA.
Uhamiaji Queens waliovaa nyeusi wakipambana na wanaume kombaini, Uhamiaji ilichapwa
Wanaume wakionyesha umahiri wa kucheza netiboli.
  Chama cha mpira pete mkoa wa Dar es Salaam (CHANEDA) kimetambulisha uongozi wake mpya kwa kufanya bonanza la mchezo huo  lililofanyika katika viwanja vya harbours view Kurasini jijini Dar es Salaam.
 
 Viongozi wapya waliotambulishwa ni pamoja Winfrida Emanuel-Mwenyekiti, Pilly Mogella-Makamu Mwenyekiti, Joseph Ng'anza-Katibu, Christina Kimamla-Katibu msaidizi, Anita Hangoli-Mweka hazina na Mauris Michael-Afisa 
 
Bonanza hilo lilishirikisha timu sita na mbili zikiwa za wanaume lilianza saa nane mchana juzi.

Awali akizungumza na wanamichezo na uongozi huo mpya wa CHANEDA, mgeni rasmi ambaye ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Dar es salaam Adolf Halii aliwataka wachezaji kushirikiana na uongozi mpya na yeye atakuwa karibu nao maana hata yeye ni mchezaji wa netiboli.

"Nawapongeza wote mlioshiriki kwenye bonanza hili ila nawaomba mshirikiane na uongozi huu mpya ili tuendeleze michezo Dar es Salaam maana hata mimi nacheza netiboli nafasi ya GS", alisema Halii.
Naye Edson Abubakar anayechezea timu ya wanaume ya Kaza roho ya Kipunguni aliwataka viongozi waanzishe ligi ya netiboli ya wanaume na kusaidia vilabu ili kuvitia moyo.

Timu zilizoshiriki ni Kipunguni Queens ambayo iliifunga Kiwalani 10-3, Karaza roho ambayo iliifunga Majumba sita (wanaume) 16-10, Bandari B iliifunga Kiwalani 18-5 na Wanaume mchanganyiko wakaifunga uhamiaji 11-10.
(Chanzo Lenzi ya michezo blog)

No comments:

Post a Comment