Rais wa Barcelona
Sandro Rosell mesema hakuna nafasi ya David Villa kuondoka Camp Nou kwa mkopo
mwezi January.
Kutokana na
mshambuliaji huyo kukosa nafasi katika kikosi cha Tito Vilanova msimu huu
kimeibua tetesi nyingi juu ya kuondoka kwa mchezaji huyo na tayari vilabu
mbalimbali hususani vya ligi kuu ya nchini England Liverpool, Chelsea, Arsenal na
Spurs zikiripotiwa kumtaka mshambuliaji huyo mwenye rekodi ya ufungaji ya
Hispania.
Hata hivyo Rosell
akiongea na gazeti la ‘Catalan paper Sport’ hapo jana akiwa katika hafla ya
utoaji wa tuzo za FIFA Ballon d’Or amesema mshambuliaji huyo haendo kokote.
Messi awashukuru Tito na Abidal
Lionel Messi
akitumia nafasi ya mahojiano yake na TV baada ya kutangazwa mshindi wa Ballon
d'Or kwa mara ya nne mfululizo hakusahau kuwashukuru Tito Vilanova na Eric
Abidal kutokana na mchango wao kwake.
Baada ya
kukabidhiwa tuzo hiyo, Messi aliwashukuru watu wengi ikiwa ni wachezaji wenzake
wa klabu yake na timu ya faifa ambao walipiga kura kwake marafiki na mtoto wake
mchanga.
Dakika chache
baadaye akiongea na TV3 ya jijini Catalunya alionyesha wazi kuwashukuru kwa
hisia kubwa kocha wake Barca Vilanova na Abidal ambao bado wanaendelea kuponya
maumivu makali baada ya kuugua.
Amenukuliwa akisema
"kwa
dhati kabisa ningependa kuchangia tuzo hii na Tito na Abidal, kilichotokea kwao
ni pigo na kuwaona tunaungana tena tukifanya kazi pamoja inanipa furaha.
Hiyo ni tuzo
kubwa kuwa wamerejea kuwa nasi tena. Kwasasa Tito anatakatiwa afanye kazi ya kurekebisha
lakini bila shaka atakuwa vizuri, nilipokwenda kupokea tuzo hayo maneno yakuwa
kichwani kwangu ".
Lionel Messi
ameshinda tuzo hiyo ya Ballon d’Or baada ya kupata asilimia 41.60% ya kura zote
akiwa mbele ya Cristiano Ronaldo aliyepata asilimia 23.68% na Andrés Iniesta akipata
asilimia 10.91% ya kura zote.
Wambach, mshindi
wa tuzo kwa upande wa wanawake aliingoza Marekani nchini Uingereza katika
michuano ya Olympics 2012 jijini London, ambako huko alishinda tuzo ya mpira wa
dhahabu ya kampuni ya Adidas ‘adidas Golden Ball’ kama mchezaji bora wa
mashindano na pia tuzo ya ufungaji bora ya Adidas (adidas Golden Boot) baada ya
kupachika wavuni jumla ya magoli 5.
Amepata asilimia
20.67% ya kura zotr akiwashinda Mbrazil Marta na Alex Morgan kutoka Marekani
ambao walipata asilimia 13.50% na 10.87% ya kura zote zilizopigwa.
Vicente del
Bosque kama kocha bora wa timu ya za wanaume wa FIFA amepata asilimia 34.51% ya
kura zote akiwashinda José Mourinho, kocha wa Ureno na klabu ya Real Madrid, aliyepata
asilimia 20.49%, na kocha wa zamani wa FC Barcelona Pep Guardiola, aliyepata asilimia
12.91% ya kura zilizopigwa.
Wakati hayo
yakiwa hivyo naye Pia Sundhage amekuwa kocha wa timu za wanawake wa mwaka baada
ya kukusanya asilimia 28.59% ya kura zote akiwashinda Norio Sasaki wa Japan aliyepata
asilimia 23.83% aliyefanikiwa kupata
medali ya fedha katika michezo ya Olympics jijini London, na kocha wa timu ya
taifa ya Ufaransa Bruno Bini aliyepata asilimia 9.02%.
FIFPro, muungano
wa wachezaji wa duniani iliwaalika jumla ya wachezaji wakulipwa 50,000 kutoka
sehemu mbalimbali duniani kuchagua timu bora ya mwaka 2012 (FIFA FIFPro World
XI 2012).
Waliochaguliwa
ni pamoja na
Mlinda mlango -Iker Casillas (Spain)
Walinzi -Dani Alves (Brazil), Marcelo (Brazil), Gerard Piqué (Spain) na Sergio
Ramos (Spain)
Viungo-Xabi
Alonso (Spain), Andrés Iniesta (Spain) na Xavi Hernández (Spain)
Washambuliaji- Cristiano Ronaldo
(Portugal), Radamel Falcao (Colombia) na Lionel Messi (Argentina).
Tuzo
nyingine maarufu ilikuwa ni ‘FIFA Puskás Award’ ambayo inatoka kwa goli bora la
mwaka ambayo inapigiwa kura kupitia mtandao wa FIFA ambapo goli hilo linawekwa
katika mtandao wa FIFA.com kupitia YouTube na mtandao mwingine wa ‘francefootball.fr’
ambapo mashabiki zaidi ya milioni 5 wanawakilisha katika kulipigia kura goli
hilo.
Tuzo hiyo
kwa mara ya kwanza ilizinduliwa 2009 kwa heshima ya nyota na nahodha wa zamani
wa Hungary Ferenc Puskás, ambaye alikuwa nahodha wa Hungary miaka ya 1950.
Kwa mara ya
kwanza tuzo hiyo ilichukuliwa na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Slovakia Miroslav
Stoch, ambaye alifunga goli katika kisambusa cha ndani ya nyavu hiyo ilikuwa
tarehe 3 March 2012 akiwa na klabu yake ya Fenerbahçe katika ligi kuu ya nchini
Uturuki dhidi ya Gençlerbirliği.
Franz
Beckenbauer amepewa tuzo ya heshima ya Rais wa FIFA Joseph S. Blatter katika
kutambua mafanikio yake na rikodi yake nzuri katika soka kama mchezaji wa zamani lakini pia kama mshauri.
Tuzo ya FIFA
ya mchezo wa kiungwana ‘FIFA Fair Play Award ‘ imekwenda kwa shirikisho la soka
la Uzbekistan (UFF).
Ba: Chelsea itatwaa mataji mengine.
Demba Ba amesisitiza
kuwa ingawa Chelsea ina matumaini kidogo katika kuelekea kuchukua taji la ligi
kuu ya nchini England, lakini bado wanapaswa kujitahidi ili kushindania mataji
mengine.
Licha ya
kwamba Chelsea ina mchezo mmoja mkononi ukilinganisha na vinara wa msimamo wa
ligi Manchester United, hata hivyo Chelsea inahitaji miujiza kuvunja daraja kubwa
la alama 14 kati yao.
Baada ya
kusaini mkataba wa miaka mitatu na nusu wa kufanya kazi Stamford Bridge, Ba, mbaye
alifunga magoli mawili katika mchezo wake wa kwanza dhidi ya Southampton katika
michuano ya FA Cup, ameonekana kusema ukweli juu ya kile ambacho Chelsea
inaweza kufanya msimu huu.
Akiongea na
L’Equipe amesema
"ni
ngumu kwetu kumkamata Manchester United anayeongoza ligi lakini bado kuna
vikombe vitatu tunapaswa kujitahidi kushinda vikombe vingi ikiwezekana" Ba
told L'Equipe.
No comments:
Post a Comment