KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, February 9, 2013

OLJORO MWENYEJI WA SIMBA VPL 2012/2013

KIKOSI CHA SIMBA
KIKOSI CHA JKT OLJORO
 
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara msimu wa 2012/2013 inaingia raundi ya 16 leo jioni  (Februari 9 mwaka huu) kwa mechi nne ambapo Oljoro JKT itaikaribisha Simba jijini Arusha.

Mechi hiyo namba 129 itafanyika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid huku Simba ikiingia na kumbukumbu ya sare katika mechi yake iliyopita dhidi ya JKT Ruvu wakati wenyeji wao wakiwa wameshinda 2-0 dhidi ya Kagera Sugar.


Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba wenye uwezo wa kuchukua watazamaji 3,000 tu utatumika kwa mechi kati ya wenyeji Kagera Sugar na Mgambo Shooting. Mwamuzi wa mechi hiyo atakuwa Amon Paul kutoka Musoma mkoani Mara.
KIKOSI CHA KAGERA SUGAR

Toto Africans baada ya kufanya vibaya katika mechi tatu zilizopita ugenini imerejea nyumbaji jijini Mwanza itakapoumana na Coastal Union ya Tanga katika mchezo utaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Mwamuzi Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ndiye atakayechezesha mechi kati ya wenyeji Tanzania Prisons na African Lyon ambayo imepata huduma za kocha mpya Salum Bausi kutoka Zanzibar. Hiyo itakuwa mechi ya kwanza kwa Bausi kuiongoza timu katika VPL.

Maofisa wengine wa mechi hiyo ni mwamuzi msaidizi namba moja Abdallah Rashid, mwamuzi msaidizi namba mbili Abdallah Mkomwa wote kutoka Pwani wakati mwamuzi wa mezani ni John Kanyenye wa Mbeya. Kamishna wa mechi hiyo ni Rashid Rwena kutoka Ruvuma.

Mechi kati ya Mtibwa Sugar na Azam iliyokuwa ichezwe leo imesogezwa mbele kwa siku moja ambapo sasa itafanyika kesho Jumapili (Februari 10 mwaka huu) katika Uwanja wa Manungu ulioko Turiani mkoani Morogoro.
Kikosi cha Azam fc kesho kina kazi dhidi ya Mtibwa Manungu.


Rnk
TeamMPWDLGFGA+/-Pts
1 Young Africans15103229121733
2 Azam1593323131030
3 Simba SC1576224131127
4 Coastal Union157531915426
5 Ruvu Shooting157352017324
6 Mtibwa Sugar156541914523
7 Kagera Sugar155641615121
8 JKT Oljoro155551817120
9 Mgambo JKT155371116-518
10 JKT Ruvu154471422-816
11 Tanzania Prisons15366915-615
12 Toto African152671221-912
13 Polisi Morogoro15249616-1010
14 African Lyon1523101024-149

No comments:

Post a Comment