Kikosi cha Ashant kinakazi kesho dhidi ya Transcamp uwanja wa Karume. |
Ligi
Daraja la Kwanza (FDL) kuwania tiketi za kucheza Ligi Kuu ya Vodacom
(VPL) msimu ujao inaendelea kutimua vumbi wikiendi hii kwa mechi kumi na
moja zitakazopigwa kwenye viwanja mbalimbali.
Kundi
A kesho (Februari 10 mwaka huu) Mbeya City itacheza na Polisi
Iringa katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Mkamba
Rangers itaumana na Burkina Faso (Uwanja wa CCM Mkamba) wakati JKT Mlale
itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Green
Warriors na Ndanda zinacheza hii leo (Februari 9) kwenye Uwanja
wa Karume, Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B. Mechi
nyingine kundi hilo leo ni kati ya Tessema na Villa Squad kwenye
Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Kesho(Februari 10)Transit Camp itacheza na Ashanti United kwenye
Uwanja wa Karume, Dar es Salaam wakati Polisi Dar es Salaam na Moro
United zitavaana Uwanja wa Mabatini mjini Mlandizi.
Kundi
C kesho (Februari 9 mwaka huu) ni Polisi Dodoma vs Polisi Tabora
(Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Polisi Mara vs Mwadui (Uwanja wa Karume,
Musoma), Morani vs Kanembwa JKT (Uwanja wa Kiteto, Manyara) na Rhino
Rangers vs Pamba (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora).
No comments:
Post a Comment