Wachezaji wa Kili taifa Stars mara baada ya mazoezi asubuhi ya leo. |
Wachezaji wa
wawili wa Yanga Kelvin Yondan na Frank Domayo sasa watalazimika kuelekea moja
kwa moja nchini Ethiopia wakitokea nchini Uturuki kuungana na wachezaji wengine
wa timu ya taifa ‘Kili taifa stars’ ambayo inaondoka nchini mchana wa leo kuelekea
nchini humo kwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya nchi
hiyo mchezo ambao umepangwa kufanyika keshokutwa tarehe 11/01/2013.
Hayo yameelezwa
na meneja wa timu ya taifa Leopard Tasso Mukubezi alipokuwa akiongea na
Rockersports asubuhi hii wakati stars walipokuwa wakifanya mazoezi ya mwisho
mwisho kabala ya safari mchana wa leo.
Taso amesema
Kelvin Yondani na Frank Domayo wameshindwa kupata usafiri wa kuwaleta nchini na
kuwahi safari na wenzao hivyo wamelazimika kubadilisha safari ya nchini Tanzania
na sasa watakuwa safarini wakielekea nchini Ethiopia.
Kocha wa
Kili taifa stars Kim Poulsen kupitia shirikisho la soka nchini TFF aliwaomba
wachezaji wawili kati ya watano wa Yanga ambao wako katika kikosi cha Yanga
kinachoendelea na kambi Antalya nchini Uturuki ili kuongeza nguvu katika kikosi
cha timu ya taifa kitakacho cheza na Ethiopia.
Wachezaji wengine
wa stars kutoka Yanga ambao wamesalia Antalya ni Nadir Haroub Kanavaro,
Athumani Iddi Chuji na Simon Msuva ambao taarifa zinasema wataungana na kambi
ya Kili taifa stars mara baada ya Yanga kumaliza ziara yao ya kambi nchini
Uturuki.
Wachezaji
watatu wa Azam Salum Abubakar, Mcha Khamis na Aishi Manula wao walijiunga na kambi
ya timu ya taifa tangu jana na leo wameshiriki mazoezi ya asubuhi kabla ya safari
ya Ethiopia mchana wa leo.
Mpaka sasa
kambi hiyo ina jumla ya wachezaji 16 wakiwepo wachezaji wengine kutoka Simba
Juma Kaseja, Mrisho Ngasa, Amri Kiemba, Amir Maftaha, Mwinyi Kazimoto na
Shomari Kapombe.
Wengine ni
Aggrey Moris na Erasto Nyoni wa Azam fc ambao walijiunga na kambi hiyo tangu
mapema kwakuwa wapo jijini Dar es Salaam kutokana kusimamishwa na klabu yao ya
Azam kwasababu za kuhusishwa na tuhuma upangaji wa matokeo.
Wachezaji wengine ni Shabani Nditi , Issa Rashid
wa Mtibwa, Mbwana Samata na Thomas
Ulimwengu wa TP Mazembe timu ya Taifa itaondoka kesho saa tisa kwa mchezo mmoja
dhidi ya Ethiopia tarehe 11/01/2013 ukiwa ni mchezo wa maandalizi ya mchezo
wake wa kuwania fainali ya kufuzu kombe la dunia mwezi machi dhidi ya Morocco.
Wao Ethiopia
wanajiandaa kwa ajili ya fainali za mataifa ya Afrika nchini Afrika kusini na
wanatarajia kuanza mchezo wao wa kwanza dhidi ya mabingwa wa soka barani Afrika
Zambia tarehe 21 mchezo wa kundi C katika uwanja Mbombela.
No comments:
Post a Comment