KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 8, 2013

ROCKERSPORTS SET AGENDA: NATAMANI RAIS KIKWETE UTUACHE NA MPANGO WA UWANJA MWINGINE MKUBWA KAMA ALIVYOFANYA MZEE BENJAMINI. RAHA YA MICHEZO VIWANJA.

Hivi ni viwanja vya soka nchini Afrika Kusini ambavyo vina hadhi na kukidhi mahitaji yote muhimu ikiwemo miundo mbinu na vifaa vyote muhimu vya kimichezo.
Viwanja hivi vitatumika katika michezo ya AFCON 2013 kuanzia Januari 19. 
Uwanja wa Soccer City.




Uwanja wa Moses Mabhida.
Uwanja wa Nelson Mandela Bay.
 Uwanja wa Mbombela.
Uwanja wa Royal Bafokeng.
 Wakati mwingine nimekuwa nikitamani kumwambia ana kwa ana endapo nitapata fursa ya kufanya hivyo au hata kumwambia kwa maandishi kupitia barua pepe na hata kupitia ujumbe mfupi wa maneno kupitia simu yake ya kiganjani kuwa Mheshimiwa Rais Dr Jakaya Kikwete tafadhali sana tena sana kabla ya kuondoka ikulu tamka maneno ambayo yatawafurahisha wananchi wote ambalo ni uwanja mwingine wa michezo kama wa TAIFA.

Bila kujali mtazamo wa mtu mmoja, muono na utashi wa utofauti katika masuala ya maendeleo maana kila mtu ana fikiri namna akili yake inavyomtuma na kutenda mambo vile aonavyo na anavyo tafsiri neno maendeleo.

 Kwangu mimi nikiwa nawakilisha mawazo ya watu wenye matazamo chanya kama wangu kuhusu maendeleo ya michezo basi mheshimiwa tuwekee mipango ya ujenzi wa uwanja mwingine mkubwa wa michezo kama uwanja wa Taifa wa pale Chang'ombe jijini Dar es Salaam kama alivyofanya mzee Benjamini Mkapa Rais wa awamu ya tatu na wewe mheshimiwa ukaja ukamalizia.

Kwa kweli sasa hivi wanamichezo unapomtaja vibaya mzee Benjamini Mkapa kuhusu maendeleo ya michezo nchini, wako tayari kukupiga kutokana na raha wanazopata wanapokwenda uwanjani wakiwamilia zao na hali ya usalama ni ya swafi.

Jambo la kufurahisha ni kwamba huwezi kabisa ukalinganisha na enzi za shamba la bibi yaani uwanja wa Uhuru ambapo watu wanafurika jukwaani na mijasho chapwachapwa na usishangae baadaye mtu anakuuliza hivi goli limefunga na nani licha ya kwamba mlikuwa wote uwanjani.

Ahsante mzee Mkapa kwa hilo mungu akupe afya njema na ikiwezekana uwe unakuja uwanjani kuaangalia mpira siku moja moja tukifurahia pamoja mchezo wa soka na hata michezo mingine.

Imani ya Wanzania ni kwamba mheshimiwa Kikwete ni mdau mkubwa wa michezo umefanya mengi katika kujaribu kuendeleza michezo hapa nchini katika kipindi chako cha uongozi ambacho bado kinaendelea.

Ndoto yangu basi kwamba ni siku moja Rais Kikwete utatamka kiwanja kingine, na utaweka jiwe la msingi kabisa ili yule utakaye mkabidhi kijiti mwaka 2015 ajue kuwa ana jukumu la kumalizia uwanja huo wa michezo na tutapima kasi ya utekelezaji wake.

Please over please Mr. President timiza ndoto yangu ya uwanja mwingine wa michezo  hapa nchini wenye hadhi angalau kama uwanja wa Taifa na ikiwezekana ujengwe makao makuu ya nchi Dodoma kama ulivyo uwanja wa Loftus Versveld ulioko Pretoria nchini Afrika Kusini ikishindikana basi jijini Dar es Salaam kwa mara nyingine tena kwa maana ya jijini la kibiashara zaidi.

Wakati naliomba hilo kwa Mr President ningependa pia kuipongeza klabu ya Yanga kwa kuwa na mpango wa ujenzi wa uwanja wao pale Jangwani kama ambavyo mwenyekiti wa Yusuph Manji alivyo weka wazi mpango huo mwaka jana. hilo ni jambo la kupongezwa na la kuungwa mkono.

Azam nao wako katika mpango wa ujenzi wa uwanja mkubwa tofauti na uwanja wa mazoezi unaotumika sasa na ambao umesaidi timu mbalimballi katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Zipo faida nyingi endapo kama tutakuwa tayari na viwanja hivyo, kwanza tutaweza kwa urahisi kulishawishi shirikisho la soka Afrika CAF kuandaa fainali za michuano mikubwa kama AFCON kama ilivyo kwa Misri na Afrika kusini ambao sasa wanapokezana kuandaa fainali hizo.

Jambo la pili ni kujenga hamasa katika kukuza michezo nchini kwa vijana na wadau wengine wa michezo kuongeza chachu ya michezo si tu mchezo wa mpira wa miguu bali pia hata michezo mingine ikiwemo kikapu, mpira wa mikono, riadha, Boxing na kadhalika kwa kuwa viwanja hivyo vina hadhi ya Olympic vinauwezo wa kubeba michezo ya aina zote. 

Nawasilisha. 
Mandhari ya uwanja wa Taifa ukiwa ndani ya  uwanja wa Uhuru.
 Mandhari ya uwanja wa Taifa unaovyoonekna kwa ndani.

No comments:

Post a Comment