Mshambiliaji Mrisho Ngasa akijiandaa kupiga mpira uliozaa goli dhidi ya Zambia mwezi Disemba uwanja wa Taifa. |
Mabingwa wa
soka barani Afrika Zambia wamejikuta wakiendelea kuadhibiwa katika mchezo wa
tatu mfululizo wa kirafiki ikiwa ni katika muendelezo wake wa kupasha moto
misuli kuelekea katika fainali za mataifa ya Afrika AFCON 2013.
Mara hii
jumapili wakiwa katika dimba la Dobsonville jijini Johannesburg Chipolopolo walizamishwa tena timu
ya taifa ya Angola Palancas Negras kwa mabao 2-0.
Mshambuliaji
anayechezea soka katika klabu ya Parana inayoshiriki ligi daraja la pili Geraldo,alianza
kufunga goli la kwanza kunako dakika ya 8 na mlinzi Amaro anayechezea Primeiro
Agosto ya Angola akifunga goli la pili zikiwa zimesalia dakika 5 mchezo
kumalizika.
Zambia ambao
ndio watetezi wa taji wataanza fainali za mataifa ya Afrika January 21 dhidi ya
Ethiopia katika mji wa kaskazini mashariki nchini Afrika Kusini wa Nelspruit.
Kabla ya
mchezo wao wa juzi dhidi ya Angola, mabingwa hao watetezi walianzia michezo yao
ya kujipima nguvu nchini Saudi Arabia ambako walifungwa kabla ya kukanyaga ardhi
ya Tanzania na kupata kichapo kingine kutoka kwa timu ya taifa ya Tanzania(Taifa
Stars) mwezi uliopita.
Katika mchezo
huo Herve Renard aliwatumia wachezaji 22 ambapo kipindi cha kwanza aliwatumia
11 kabla ya kubadilisha wote kipindi cha pili kwa lengo la kujaribu wachezaji
wake 23 kabla ya fainali za mataifa ya Afrika kuaanza katika kipindi cha wiki
mbili zijazo.
Kipindi cha
kwanza aliwatumia mlinda mlango Kalililo Kakonje , Davies Nkausu, Stoppila
Sunzu, Hichani Himoonde, Joseph Musonda, Mukuka Mulenga, Shadreck Malambo,
Isaac Chansa, Rainford Kalaba, Collins Mbesuma na Chris Katongo.
Kipindi cha
pili aliwaingiza Kennedy Mweene GK, William Njobvu, Salulani Phiri, Francis
Kasonde, Emmanuel Mbola, Nathan Sinkala, Noah Chivuta, Chisamba Lungu, Felix
Katongo, James Chmanga na Jonas Sakuwaha.
Hata hivyo
matokeo hayo mabaya ya michezo ya kujipima nguvu hayamsumbui kocha mfaransa
mwenye umri wa miaka 44 Herve Renard kwa kuwa Zambia pia ilikuwa na matokeo
mabaya ya michezo ya kujipima nguvu katika fainali zilizopita kabla ya kushinda
taji mbele ya waliokuwa wanapewa nafasi kubwa tembo wa Ivorycoast.
Kumbuka katika jumla ya michezo mitatu waliyocheza hawajafunga goli hata moja kutokana na uwezo mdogo wa washambuliaji walioko kambini hivi sasa huku washambuliaji tegemeo Jacob Mulenga wa FC Utrecht ya Udachi na Emmanul Mayuka wa Southamptom ya England wakitarajiwa kuwasili hii leo.
Chipolopolo bado
ina michezo kadhaa ya kirafiki katika programu yao ambapo inataraji kucheza dhidi
ya Morocco, Norway na Namibia kabla ya kulivaa kundi C la michuano ya AFCON
2013 ambalo lina timu za Ethiopia, Nigeria na Burkina Faso.
Hebu tuangalie mchezo wa kesho dhidi ya Morocco wakiwa na wakali hao tuone kama mambo yanaweza kubalidilika.
Angola ambao
wako katika kundi A pamoja na wenyeji Afrika Kusini, Morocco na Cape Verde
Islands, ikiwa chini ya kocha raia wa Uruguay Gustavo Ferrin kwao huo ulikuwa
ni ushindi wa tatu katika mfululizo wa michezo yao ya kujipima nguvu baada ya
kutangulia kuzichapa Rwanda na Cameroon.
Akitoa salamu zake za mwaka mpya kwa watu wa Zambia Rais wa chama cha soka cha Zambia FAZ mbaye aliwahi kuwa mchezaji bora wa Afrika mwaka 1988 ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Afrika Kalusha Bwalya alisema maneno ambayo ni katika kipindi cha siku tano kipindi kifupi tu kabisa tayari watu wa Zambia wameanza kukata tamaa.
Katika salamu hizo alisema,
"New Year will be excellent as Chipolopolo attempt to
defend her Nations’ Cup crown as well as secure an unprecedented place
at the Fifa World Cup finals".
“The Nations Cup finals will be tough but we are toughened and we shall be ready,”
“We also have Fifa World Cup qualifiers to complete. The dream of every
Zambian is one day to see our own lads at the finals. It's a long and
difficult road which we shall tackle one match at a time and by the turn
of the year, we can all hopefully dream of trekking across the Atlantic
to Brazil,”
Kwa heshima ya Kalusha Bwalya nchini Zambia kama ilivyo kwa Leodigar Chila Tenga wa Tanzania, hayo ni maneno mazuri lakini kama yatakwenda na vitendo ambavyo moja kwa moja na matokeo ya uwanjani haijalishi ni mchezo wa kirafiki au wa kimashindano kikubwa ni matokeo yakupendeza kwa wadau wasoka ndani ya Zambia na nje ya mipaka ya Zambia.
Ukisoma maoni yao Zambia wenyewe waliotuma kupitia mtandao wa chaka cha soka cha Zambia utapata picha tofauti kwani wapo wanao ona kwamba timu yao itatetea taji lakini kuna wengine wameshakata tamaa.
NA HAYO HAPO CHINI NI MAONI YA WAZAMBIA WENYEWE KUPITIA MTANDAO WA CHAMA CHA SOKA CHA ZAMBIA JUU YA MWENENDO WA TIMU YAO KABLA YA AFCON KUANZA.
Philip Wilson
Guys lets not worry much about the results of these friendly games. In as much as we all want to see our team win, I think I for 1 I would rather see them loose these friendlies because that will give the technical bench a good and clear picture of where we are lucking before the tournament start. Am sure if they do so and work on those weaknesses, we will be a force to recon with at the tournament. If we win these friendlies I can assure you that we will grow big headed and think we have all done. If there is 1 game I would want us to win of all the lined up games is that for Norway. Not that its a European team but because it will be at home and they guys will be biding farewell to that nation so its better they go win a win. Objective soccer fan.
Henry Sten MK · Solusi University
you right. I am of the same view. Looking at the team they used, they were trying to avoid Injuries in this time that is so much reduced. My worry is Ethiopia, Those guys scored 5goals against Sudan-which not even Ivory Coast can manage. The policy is avoid injuries and fool the opponent. I know everyone wants us,but the current result works on two sides: First, it shows that there is still a lot of work to be done within the team and second the enemies, Especially Ethiopia and Nigeria will take Zambia as an average team.
Ayew has been rule out of the AFCON and we want to avoid that bacause we have very few players.
with Chisamba, Mayuka and Jacob, the volume of the team is increasing.
Go boys and swallow them up all!
Nchi Munya · Training Officer at Ministry of Agriculture
Great that rainford is getting some game time. Can't wait for the games to begin Im sure we will be a force in the tournament
Evans Mulenga · Assistant Internal Auditor at Workers' Compensation Fund Control Board
I HOPE THIS IS NOT A TRUE REFLECTION OF THE CALIBER OF OUR SOCCER SQUAD THAT IS GOING TO DEFEND THE CUP.
No comments:
Post a Comment