KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Real Madrid Carlo Ancelotti: Ronaldo alistahili ushindi wa Ballon d'Or na atafanya vizuri pia 2014

 Kocha wa Real Madrid Carlo Ancelotti amempongeza mshambuliaji wa Real Madrid na nahodha wa Ureno Cristiano Ronaldo na kusema kuwa mpira wa miguu inamuhitaji mchezaji kama Ronaldo.

Mdhambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 usiku wa jana alimshinda mpinzani wake Lionel Messi kutwaa tunzo ya uchezaji bora ya Fifa ya Ballon d'Or kwa mwaka 2013 katika hafla iliyofanyika Zurich.
 Ancelotti anadhani mshambuliaji huyo mwenye uwezo mkubwa alistahili kuchukua tunzo hiyo kufuatia ubora wa uchezaji wake nidhamu yake ya kweli kama Professional .

Amekaririwa kocha huyo wa Madrid akisema katika mkutano wake na wanahabari
"Sikushangazwa na ushindi wake kutokana na ubora wa soka lake na aina ya magoli yake anayofunga, lakini pia U-professionalism anayoonyesha anapokuwa ndani na nje ya uwanja haikunishangaza mimi. Ni mfano wa kuigwa kwa wachezaji wachanga"

"Football inahitaji mchezaji kama Ronaldo. Ni mchezaji mwenye uchezaji wa uungwana na amejidhatiti. Anaonyesha taswira nzuri katika mpira wa miguu, kama ilivyo pia kwa nyota wengine kama Lionel Messi, Franck Ribery, Thiago Silva na Andrea Pirlo.

"Ronaldo ana vitu vyote kipaji na kujituma. Katika soka la kisasa hutakiwi kutegemea kipaji peke yake. Kipaji unazaliwa nacho, lakini pia unatakiwa ujitume. Wote tumefurahia ushindi wake wa Ballon d'Or. Anastahili."

Ancelotti akaenda mbali zaidi kwa kusema Ronaldo anaweza kufanya vizuri zaidi mwaka huu wa 2014 baada ya kuwa tayari amesha tupia jumla ya mabao 69 katika michezo ya mashindano yote mwaka uliopita.

Ronaldo amesha funga mabao mawili katika michezo mitatu aliyocheza tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2014.

No comments:

Post a Comment