KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Coastal Union dhidi ya Oman Club uwanja wa Nadi Oman huko Boshra Muscat

LEO timu ya Coastal Union itashuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Oman Club, katika uwanja wa Nadi Oman katika wilaya ya Boshra jijini Muscat.
Hiyo inakuwa mechi ya pili tangu kuwasili huko Januari 9, kwa kambi ya wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili ligi kuu ya Tanzania bara.
Katika mchezo wa kwanza Coastal Union, walicheza na Al Musannah inayoshiriki ligi ya Oman, ambapo Wagosi wa Kaya wliibuka na ushindi wa mabao 2-0 ambayo yalifungwa na Yayo Kato na Kenneth Masumbuko.
Aidha Wagosi wa Kaya wakiwa wanaendelea na ziara hiyo ya maandalizi yao wanatarajia kucheza mchezo mwingine na timu ambayo mwenyeji mwenyeji wao Twalib Hilal, amewaahidi kuwapatia ya timu ya daraja la chini ili Kocha Yusuf Chipo, aweze kuwajaribu vijana wake wa U20 waliopandishwa msimu huu.
Timu nne zilizopangwa awali ni Al Musannah Club, Oman Club, Seeb Club na Fanja Club, timu zote tatu zipo ligi kuu ya Oman, isipokuwa Oman Club yenyewe inashiriki ligi daraja la kwanza nchini Oman maarufu kama Professional League.
Kikosi cha leo kitakachocheza na Oman Club, saa kumi na nusu alasiri ni: Said Lubawa, Ayoub Masoud, Othman Tamim, Marcus Ndeheli, Yusuf Chuma, Razak Khalfan, Ally Nassor ‘Ufudu’, Behewa Sembwana, Suleiman Kassim ‘Selembe’, Mohammed Miraji, na Othman Abdullah ‘Ustadh’.
COASTAL UNION
14 JANUARI, 2014
MUSCAT, OMAN

No comments:

Post a Comment