KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

TFF YATEUA KIKOSI CHA UKAGUZI WA VIWANJA VYA LIGI KUU NA DARAJA LA KWANZA

Sehemu  ya kuingilia ndani ya uwanja kumbukumbu ya Sokoine
Sehemu ya kuchezea ya uwanja wa Ally Hassani Mwinyi mkoani Tabora
Hii ndio sehemu ya kuingilia uwanjani sehemu ya VIP ya uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine ulioko mkoani Mbeya

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeteua maofisa wanaoanza leo (Januari 14 mwaka huu) kukagua viwanja 19 vitakavyotumika kwa mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL).

Ukaguzi huo pia unahusisha viwanja ambavyo Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) ilizuia mechi za VPL na FDL kuchezwa mpaka hapo vitakapokuwa vimefanyiwa marekebisho ili kukidhi sifa za kutumiwa kwa mechi hizo.

Viwanja vinavyokaguliwa ni Ali Hassan Mwinyi (Tabora), CCM Kirumba (Mwanza), Jamhuri (Dodoma), Jamhuri (Morogoro), Kaitaba (Bukoba), Kambarage (Shinyanga), Kumbukumbu ya Karume (Musoma) na Kumbukumbu ya Samora (Iringa).

Kumbukumbu ya Sokoine (Mbeya), Lake Tanganyika (Kigoma), Mabatini (Pwani), Majimaji (Songea), Mbinga (Mbinga), Mkwakwani (Tanga), Mwadui (Shinyanga), Wambi (Mufindi, Iringa), Sheikh Kaluta Amri Abeid (Arusha), Umoja (Mtwara) na Vwawa (Mbozi).

Vyama vya mpira wa miguu vya mikoa husika na mameneja wa viwanja husika wanatakiwa kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kutoka TFF.

No comments:

Post a Comment