KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Winga wa zamani wa Liverpool Luis Garcia astaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 35.

Winga wa zamani wa Liverpool Luis Garcia amestaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 35.
Garcia awasaidia wekundu wa Liverpool kushinda taji la ligi ya mabingwa Ulaya mwaka 2005 huku Liverpool ikifanya kazi ya ziada kuishinda AC Milan ikitokea nyuma kimatokeo ya 3-0 kabla ya kuanza kuandika bao moja baada ya lingine na kufanikiwa kusawazisha na hatimaye kuwashinda wapinzani wao kwa njia ya penati.
Winga huyo wa zamani wa Hispania aliwahi kuvitumikia vilabu vya Atletico Madrid na Barcelona kabla ya kujiunga na Liverpool mwezi Agosti 2004.
Pia aliiwahi kutoa huduma katika vilabu vya Racing Santander, Panathinaikos na Puebla kabla ya kumalizia soka yake katika klabu noja ya huko Mexico ya Pumas UNAM.

Garcia akiwa Liverpool

Luis Garcia alijiunga na Liverpool Agosti 2004 na kuifungia jumla ya magoli 30 katika michezo 121 aliyoichezea Liverpool. 

Kuelekea kushinda taji Ulaya mwaka 2005 akiwa na Liverpool, Garcia ambaye aliichezea timu ya taifa ya Hispania jumla ya michezo 20 alifunga goli muhimu lililozua mzozo dhidi ya Chelsea katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali.

Jose Mourinho, ambaye alikuwa katika klabu ya Chelsea kwa mara ya kwanza kama meneja wa timu hiyo alilalamikia goli hilo akidai kuwa mpira wa Garcia haukuvuka mstari wa goli.

Garcia anastaafu akiwa na kumbukumbu nzuri ya kutakata ya kushinda mataji kadhaa ikiwa ni pamoja na Super Cup mwaka 2005 na FA Cup mwaka 2006 katika misimu yake mitatu aliyotumikia katika viunga vya Anfield.

No comments:

Post a Comment