KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 14, 2014

Wakati Real Madrid ikiweka tofauti ya alama tatu na vinara wa La liga Barca na Atletico, hii ni timu ya wiki ya La liga.

Mwishoni mwa juma katika ligi kuu ya nchini Hispania kumefanyika michezo kadhaa ya ligi hiyo takribani michezo kumi ya 'Primera Division' ambayo kimsingi yalibadilisha msimamo wa ligi hiyo ambayo ilifikia katikati ya msimu rasmi.

Real Madrid ilifanikiwa kuwakaribia vinara wa ligi hiyo Barcelona na Atletico Madrid walioko kileleni mwa msimamo huo wakiwa na alama 50 kila moja, na baada ya suluhu baina ya timu hizo mbili maarufu kama Catalans na los Colchoneros mchezo uliopigwa Vicente Calderon Jumamosi, kikosi cha Carlo Ancelotti kiliitumia faida hiyo ya suluhu kwa kuwakandamiza Espanyol siku iliyofuatia.

Kwingineko, Athletic Bilbao akafanikiwa kuifumua Almeria bao 6-1 na Villarreal wakawagonga watakavyo Real Sociedad kwa mabao 5-1, ilhali Granada, Celta Vigo, Osasuna na Levante nao wakashinda michezo yao.

Rockersports inakuletea kikosi cha wiki kufuatia viwango vilivyoonyeshwa na wachezaji wa timu zote ambao wanastahili kuwa bora katika kikosi cha wiki hii baada ya roundi hiyo ya 19 kukamilika.

Goli kipa ni Keyla Navas, yeye alivutiaa wakati Levante alipopigana kuwashinda Malaga kwa bao 1-0 Levante wakiwa ugenini, huku Pepe akionekana kukuza ugumu wa ukuta wa Real Madrid walipopata ushindi wa bao 1-0 la kujifunga wenyewe wapinzani wao Espanyol.
 
Daniel Carrico alikuwa shujaa wa Sevilla kufuatia kufunga goli la dakika za mwisho na kufanikisha sare dhidi ya Elche, wakati ambapo Jeison Murillo alionyesha ubora wake katika kikosi cha Granada ambacho kilishinda bao 4-0 dhidi ya Valladolid.

Ander Herrera na Mikel Rico walikuwa bora katika sehemu ya kiungo ya kikosi cha Athletic Bilbao kilichoibuka na ushindi wa mabao 6-1 ilhali Moi Gomez akitakata katika kikosi cha Villarreal kilichoshinda Jumatatu, naye Recio akichagiza ushindo wa mabao 4-0 wa Granada yeye peke yake akifunga mabao mawili nyumbani kwa Valladolid.

Katika ushambuliaji, mshambuliaji Charles aling'ara baada ya kuifungia Celta Vigo mabao mawili, wakati ambapo Ikechukwu Uche na Giovani dos Santos wakifunga mabao manne wao wawili na kuchagiza ushindi wa Villarreal dhidi ya Real Sociedad na kuendeleza ubora wao wa hivi karibuni.
 
Hilo ndio kosi la wiki la La liga.

No comments:

Post a Comment