Kiungo wa Manchester
City Yaya Toure amesema lengo lake ni kumalizia soka yake katika klabu yake ya
sasa ya Manchester City ambao ndio mabingwa soka nchini England.
Kiungo huyo
mwenye umri wa miaka 29 raia wa Ivory Coast amekuwa kivutio kikubwa cha kocha Roberto
Mancini tangu kuwasili kwake ndani ya klabu hiyo mwaka 2010 akitokea kwa kigogo cha
nchini Hispania Barcelona.
Amenukuliwa Toure
alipokuwa akiongea na gazeti la L’Equipe akisema,
"katika
maisha sio pesa tu, lakini pia wazazi na familia, tangu niwasili hapa nimekuwa
nikipata mshahara mzuri lakini si kwamba napata kila kitu".
"kwa
kuwa nimetokea katika klabu ya Barcelona nikiwa na historia nzuri nikafika City kwa umuhimu mdogo, lakini kitu kimoja
ambacho nakitaka ni kuandika ni historia. Naweza kuweka historia hapa City. Nina uhakika
na hilo nitakapo kuwa mtu mzima watu siku moja watanizungumzia.
"nataka
kumalizia soka yangu Manchester City kwa heshima kutoka kwa mashabiki lakini
katika soka huwezi kujua ya baadaye."
Luis Suarez ndiye Lionel Messi wa Liverpool
anasema Brendan Rodgers
Bosi wa Liverpool
ya nchini England Brendan Rodgers amemuelezea mshambuliaji wake Luis Suarez kuwa
anafanana na kiuwezo Lionel Messi baada ya kuonyesha soka safi katika mchezo dhidi ya Newcastle.
Suarez alifunga
goli zuri la kusawazisha katika mchezo huo huku akionyesha kiwango safi ndani
ya muda wote wa mchezo ambao ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 mchezo aambao ulipigwa Anfield.
Amenukuliwa Rodgers
na Sky akisema,
"amecheza
kwa majukumu nane tofauti ndani ya kiwanja kama anavyo fanya Messi katika klabu yake ya
Barcelona ambaye anatembea akiwa huru uwanjani na wengine wakimfuata nyuma
kujaribu kupenya".
"goli
la Suarez lilikuwa goli safi la kupendeza. Ni mshambuliaji wa kiwango cha dunia."
Suarez alikuwa
tishio kubwa wakati wa mchezo huo akiwapa tabu wapinzani sehemu yao ya ulinzi
na kiungo huku utembeaji wake uwanjani na upenyeshaji wake wa mipira ukiwapa tabu
wapinzani.
Shearer: Arsenal inaendelea kutereza.
Alan Shearer
amelaumu kiwango kibovu cha Arsenal walicho kionyesha katika mchezo dhidi ya Manchester
United na kudokeza kuwa klabu hiyo si muda mrefu itapoteza hadhi yake kama
klabu kubwa ya kuogopa duniani hasa kutokana na rekodi yake mbaya ya hivi
karibuni.
Kipigo kutoka
kwa United kilikuwa ni kipigo cha tatu katika msimu huu wa ligi huku mshambuliaji
wake wa zamani Robin van Persie akifunga goli la uongozi baada ya kufanyika
makosa yaliyosababishwa na mlinzi Thomas Vermaelen.
Amenukuliwa Shearer
na The Sun akihoji
"hivi
ni klabu gani duniani itaendelea kukaa na meneja ambaye hana taji hata moja
ndani ya kipindi cha miaka saba na nusu? Au ni Arsenal pekee inayojiweka katika
kundi la kipekee".
"mnafarijika
kuona wachezaji bora wakiondoka katika mazingira ambayo mna uwezo nayo, hii
inatisha na mbaya zaidi hakuna wakuchukua nafasi yake."
Shearer anaamini
kuwa Theo Walcott atafuata nyayo za nyota wengine wakubwa ambao waliihama klabu
hiyo ndani ya kipindi cha miaka minne iliyopita.
Ameendelea kwa
kusema
"watu
kama Van Persie, Cesc Fabregas, Samir Nasri, Gael Clichy, Kolo Toure na hivi
punde atakuwa Theo Walcott.
"Vina
saba (DNA) vimeondoka ndani ya klabu.
Arsenal inaonekana kuporomoka katika hatua ambayo sasa wanaonekana kama si
washindani tena wa mataji."
YAYA TOURE KUONGOZAORODHA YA KUWANIA TUZO YA MCHEZAJI BORA AFRIKA YUKO PIA KATONGO WA ZAMBIA
Cris Katongo nahodha wa Zambia. |
Kiungo raia
wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City Yaya Toure ni miongoni mwa wachezaji
wanne wanaocheza soka nchini England waliotajwa kuwania tuzo ya mwanasoka bora
barani Afrika kwa mwaka 2012.
Kiungo wa Chelsea
John Obi Mikel, mshambuliaji wa Arsenal Gervinho na mshambuliaji wa Newcastle United
Demba Ba ni wachezaji wengine kutoka katika ligi kuu ya nchini England ‘Premier
League’ waliojumuishwa.
Pia katika
orodha hiyo kuna wachezaji wengine kadhaa walio wahi kucheza soka nchini England mwaka huu wa 2012.
Wachezaji hawa
ni pamoja na kiungo wa zamani wa Arsenal Alexandre Song, ambaye kwasasa
anachezea Barcelona pamoja na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba
ambaye kwasasa anachezea klabu ya Shanghai Shenhua ya nchini China.
Chris
Katongo ni mchezaji pekee kutoka kwa mabingwa wa soka barani Afrika Zambia.
Younes
Belhanda raia wa Morocco naye ameorodheshwa katika orodha hiyo fupi kutokana na
mchango wake mkubwa katika klabu yake ya nchini Ufaransa ya Montpellier ambayo
inashiriki ligi soka ya nchi hiyo maarufu kama Ligue 1.
Wachezaji
hao watapunguzwa mpaka kufikia watatu katika wiki ya mwisho ya mwezi Novemba.
Caf pia
imetangaza orodha fupi ya wachezaji wanaocheza soka barani Afrika kwa ajili ya
kuwania tuzo ya wachezaji wa ndani ya Afrika.
Miongoni mwao
ni pamoja na kiungo wa Misri Mohamed Aboutrika, ambaye alicheza katika mchezo
uliomalizika kwa sare ya 1-1 baina ya Al Ahly na Esperance ukiwa n I mchezo wa
kwanza wa fainali uliopigwa jumapili.
Tuzo hizo
pia zinajumuisha tuzo ya kocha bora na klabu bora ya mwaka ambapo sherehe za
utoaji tuzo hizo ambazo zitafanyika Desemba 20 December katika ukumbi wa Banquet
katika mji mkuu wa Ghana Accra.
Orodha kamili:
Alexander
Song . Club: Barcelona (Spain) Country: Cameroon
Andre Ayew .
Club: Marseille (France) Country: Ghana
Christopher
Katongo. Club: Henan Construction (China) Country: Zambia
Demba Ba.
Club: for Newcastle United (England) Country: Senegal
Didier
Drogba. Club: Shanghai Shenhua (China) Country: Ivory Coast
Gervinho.
Club: Arsenal (England) Country: Ivory Coast
John Obi
Mikel. Club: Chelsea (England) Country: Nigeria
Pierre-Emerick
Aubameyang. Club: Saint Etienne (France) Country: Gabon
Yaya Toure.
Club: Manchester City (England) Country: Ivory Coast
Younes
Belhanda. Club: Montpellier (France) Country: Morocco
Orodha ya
wachezaji wanaocheza barani Afrika.
Mohamed
Aboutreika. Club: Al-Ahly (Egypt) Country: Egypt
Rainford
Kalaba. Club: TP Mazembe (DR Congo) Country: Zambia
Stoppila
Sunzu . Club: TP Mazembe (DR Congo) Country: Zambia
Yannick
N'Djeng. Club: Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) Country: Cameroon
Yousse
Msakni. Club: Esperance Sportive de Tunis (Tunisia) Country: Tunisia
No comments:
Post a Comment