Roger Milla amepoteza sifa yake iliyodumu kwa miaka 20 ya kuwa mchezaji aliyewahi kucheza mpira wa miguu akiwa mkubwa kuliko wote katika historia ya soka barani Afrika katika soka la kimataifa.
Roger Milla alicheza soka akiwa na umri wa miaka 42 huku rekodi hiyo ikivunjwa na mshambuliaji wa Mauritius mwenye umri wa miaka 43 Kersley Appou.
Mcameroon Roger Milla aliweka rekodi hiyo wakati akifunga goli katika mchezo waliopokea kipigo cha mabao 6-1 kutoka kwa Urusi katika fainali za kombe la dunia mwaka 1994 akiwa na umri wa miaka 42 na siku 39.
Bado anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji mkongwe kuliko wote aliyewahi kucheza kombe la dunia akiwa na umri mkiubwa.
Appou alichezea Mauritius katika mchezo wa mzunguko wa awali wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika dhidi ya Mauritania ambao walifungwa siku ya Jumamosi.
Alikuwa na umri wa miaka 43 na siku 354 umri ambao bado ni mdogo ukilinganishwa na umri wa MacDonald Taylor Sr, wa visiwa vya Marekani vya Virginia ambaye anashikilia rekodi ya kucheza soka akiwa na umri wa miaka 46 na siku 217.
"I plan to continue playing,"
amesema Appou,ambaye ailiingia katika mchezo huo ambao walifungwa kwa baoa 1-0 mchezo wa mkondo wa kwanza.
Milla alicheza fainali tatu za kombe la dunia moja alikuwa ni mmoja wa nyota katika fainali ya mwaka 1990 akiwa na umri wa miaka 38.
No comments:
Post a Comment