Fainali ya Copa del Rey - Real Madrid v Barcelona
- Uwanja: Mestalla, Valencia
- Tarehe: Jumatano April 16
Wachezaji wa Barcelona ameonyesha kumuunga mkono kocha wao Gerardo Martino kucheza kufa kupona katika mchezo wa fainali ya Copa del Rey, hii ikiwa ni kauli ya msisitizo kutoka kwa nahodha Carles Puyol.
Bosi wa Barcelona raia wa Argentina Martino mwenye umri wa miaka 51, amekumbwa na ukosoaji mkubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo na wadau wengine wa soka kufuatia kichapo cha mshituko kutoka kwa timu ndogo ya Granada Jumamosi iliyopita na kuweka matumaini ya Barca kutwaa taji la ligi ya Hispania La Liga mashakani.
Kichapo hicho kimekuja siku chache baada ya ya kufungwa katika mchezo wa robo fainali ya pili wa ligi ya mabingwa Ulaya na vinara wa La Liga, Atletico Madrid na kuondolewa katika kampeni ya ligi hiyo kubwa ya ngazi ya vilabu barani Ulaya.
“Tumeungana wote na hivyo itakuwa rahisi, kikubwa kuelekea kwenye mchezo ni kuendelea kuungana”
Bosi huyo wa zamani wa klabu ya kutoka Newell, Old Boys Martino aliajiriwa kiangazi iliyopita akichukua nafasi ya mtangulizi wake Tito Vilanova, ambaye aliaachia ngazi kutokana na kubanwa na ratiba ya matibabu yake ya kansa.
Ikiwa chini ya Martino, matumaini ya Barcelona ya kutetea taji la ligi ya Hispania La Liga yamezidi kufifia, ambapo kikosi chake kimejiweka katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi huku ikisaliwa na michezo mitano.
Atletico wako na alama nne zaidi ya Barca, ambao pia wanazidiwa na wapinzani wao wakubwa Real Madrid kwa alama moja.
No comments:
Post a Comment