Droo ya hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya imefanyika leo hii ambapo Chelsea imepangwa kukutana na Atletico Madrid ilhali Real Madrid wakipangwa kukutana na Bayern Munich.
Chelsea wanapambana kuweza kupata taji la tatu ndani ya kipindi cha misimu saba ambapo wanatarajiwa kuanzi mchezo wa kwanza katika dimba la Vicente Calderon tarehe 22 Aprili, huku mchezo wa pili ukitarajiwa kupigwa siku nane baadaye
Atletico wana alama moja zaidi ya Bareclona katika kilele cha msimamo wa ligi kuu ya Hispania La Liga ambapo pia waliwachapa wapinzani wao hao katika robo fainali ya ligi ya mabingwa.
Mabingwa mara tisa wa klabu bingwa Real Madrid wenyewe watakuwa nyumbani Santiago Bernabeu dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich katika mchezo wa kwanza.
Katika Michuano ya Europa League kibibi kizee cha Turin Juventus wanatarajiwa kukutana na Benfica ilhali Sevilla wakipangwa kucheza dhidi ya timu nyingine ya Hispania inayoshiriki ligi ya nchi hiyo La Liga, Valencia.
Chelsea kwa mara ya mwisho kukutana na Atletico ilikuwa mwaka jana 2012 katika Super Cup, ambapo walifungwa jumla ya mabao 4-1 huku Radamel Falcao akifunga mabao matatu pekee yake yaani 'hat-trick' mjini Monaco.
Mara hii The Blues huenda wakakutana na mlinda mlango kijana mwenye umri wa miaka 21 Thibaut Courtois, ambaye yuko kwenye mkopo katika klabu ya Atletico akitokea Chelsea.
Iliarifia hapo kabla kuwa chini ya kipengele kimoja cha mkataba wa mkopo wa mchezaji huyo Courtois alipoelekea Hispania, Atletico itatakiwa kulipa kiasi fulani cha pesa za ada ili mchezaji huyo Raia wa Belgium aweze kuichezea klabu yake ya Atletico dhidi ya Chelsea.
Lakini hivi punde shirikisho la soka Ulaya limetoa taarifa ya ufafanuzi kabla ya droo ya hii leo wakisema kuwa Courtois ni halali kucheza mchezo baina ya timu hizo endapo watapangwa katika nusu fainali ya michuano ya mabingwa na kwamba jaribio lolote la klabu ya Chlesea la kutaka kuzuia mchezaji huyo litakuwa halina mashiko
Bosi wa Chelsea, Jose Mourinho ameshinda mara tatu dhidi ya kikosi cha Diego Simeone, Atletico wakati huo akiwa kazini katika klabu ya Real Madrid
kati ya kipindi cha Mei 2010 na Juni 2013.
Lakini hata hivyo Atletico imeonyesha nguvu kubwa katika soka nchini Hispania na Ulaya kwa ujumla msimu huu.
Kwasasa Atletico maarufu kama Los Rojiblancos wako katika mserereko wa kusaka taji kwa mara ya kwanza tangu mara ya mwisho kufanya hivyo mwaka 1996.
Katika nusu fainali nyingine, kikosi cha Carlo Ancelotti cha Real Madrid nitapaswa kuwaondoa mabingwa watetezi wa Ulaya Bayern endapo watataka kuvishwa taji kwa mara ya kumi.
"If we want to win the Champions League, we have to
beat everyone including Bayern," said Ancelotti, a two-time Champions
League winner when in charge of AC Milan.
Katika hatua nyingine mchezo wa Chelsea ligi ya Premier dhidi ya Sunderland, uliokuwa umepangwa kufanyika Jumapili ya tarehe 20 umerudishwa nyuma mpaka tarehe 19 ili kuwapa nafasi The Blues kufanya maandalizi ya mchezo wa nusu fainali wa klabu bingwa.
No comments:
Post a Comment