Kikosi imara cha wanariadha nyota ikiwa ni pamoja na anayeshikilia
rekodi ya ulimwengu Mkenya Wilson Kipsang na bingwa mara mbili wa
Olimpiki Mo Farah kitashiriki katika mbio za London marathon Jumapili
(13.04.14)
Bingwa wa ulimwengu na Olimpiki Stephen Kiprotich, bingwa metetezi wa
mbio za London Tsegaye Kebede na mwanariadha aliyeweka muda bora zaidi
katika mbio za London marathon, Emannuel Mutai, pia ni miongoni mwa
nyota watakaoshiriki huku pia Muethiopia Haile Gabreselassie akitarajiwa
kuwapa motisha kwa kuongoza katika mstari wa mbele.
Macho hata hivyo yataangaziwa Farah mwenye umri wa miaka 31 anayetaka
kuwa muingereza wa kwanza kushinda mbio za London marathon tangu Eamonn
Martin katika mwaka wa 1993. Kama tu mwenzake Mo Farah, Katika mbio za
wanawake, nyota Tirunesh Dibaba wa Ethiopia atajitosa kwa mara ya kwanza
katika katika mbio za marathon.
Dibaba atafukuzana na bingwa mtetezi wa London Mkenya Priscah
Jeptoo, na wakenya wenzake Ednah Kiplagat, bingwa wa sasa wa ulimwengu
Florence Kiplagat anayeshikilia rekodi ya ulimwengu katika mbio za half
marathon miongoni mwa wengine….Farah anasema anailenga rekodi ya kitaifa
ya mwaka wa 1985 iliyowekwa na Steve Jones aliyetumia muda wa saa mbili
dakika saba na sekunde 13.
Baadhi ya wapinzani wake wanaamini kuwa huenda ikawa vigumu kwa Farah
kushiriki mbio kubwa kwa mara ya kwanza. Wakenya Kipsang na Mutai
wanasema licha ya kwamba Farah anaweza kukimbia vyema, angestahili
kuanza na mbio ndogo.
Mwezi mmoja uliopita, Farah alianguka na kuzirai baada ya kushinda mbio
za New York marathon lakini anasisitiza yuko katika hali shwari.
Kenenisa Bekele, ambaye baada ya kuutawala ulimwengu wa mbio za mita
5,000 na 10,000 alishiriki mbio zake za kwanza za marathon wikendi
iliyopita mjini Paris na akashinda mbio hizo, jambo analosema hata Farah
anaweza kufuata nyayo zake.
Tukisalia katika riadha, wmanariadha wa mbio za masafa mafupi Mjamaica
Asafa Powell, ambaye aliwahi kushikilia rekodi ya ulimwengu yam bio za
mita 100, ameishutumu hatua ya kupigwa marufuku ya miezi 18 akiitaja
kuwa isiyokuwa ya haki.
Wakili wa mwanariadha huyo wamesema tayari watakata rufaa kuhusu hatua
hiyo iliyofanywa na jopo la Jamaica la kinidhamu linalopambana na
matumizi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni lenye wanachama watatu.
Jopo hilo liliamuru wka kauli moja kuwa Powell, hastajili kushiriki
mashindanoni baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa zilizopigwa
marufuku.
No comments:
Post a Comment