Mwamuzi mashuhuri Howard Webb huendwa akaangushwa kisifa na mameneja wawili David Moyes wa Manchester United na Brendan
Rodgers wa Liverpool ambao hivi karibuni wamekuwa wakilalamikia juu ya maamuzi ya waamuzi, lakini pamoja na kadhia hiyo ya maneno makali kutoka kwa mameneja hao, bado Webb anatajwa kuwa ndiye mwamuzi bora duniani.
Webb, ambaye aliingizwa katika mzozo wa kisifa katika maamuzi yake ambayo yalipewa jina la ‘scandalous’ na meneja wa United Moyes wiki iliyopita, ametangazwa kuwa mshindi wa tunzo ya mwamuzi bora kutoka 'International Federation of
Football History & Statistics IFFHS.
IFFHS imempa tunzo hiyo mstaafu huyo wa zamani wa jeshi la polisi wa South Yorkshire na kuwashinda Nicola Rizzol wa Italia huku Viktor Kassai wa Hungary akishika nafasi ya tatu ambapo mwamuzi wa kituruki Cuneyt Cakir akishika nafasi ya tano.
Orodha kamili ya viwango vya waamuzi ni kama ifuatavyo
Huko nyuma Webb alishinda tunzo ya ubora mwaka 2010, na baadaye mwaka 2012 akashika nafasi ya tatu kabla ya kupanda mwaka jana 2013 katika nafasi ya kwanza.
Mshindi huamuliwa na jopo la mameneja wataalamu kutoka nchi 70 ingawa katika zoezi hili la sasa walalamishi wawili Brendan Rodgers David Moyes hawakuwepo kupiga kura
No comments:
Post a Comment