Baridi: FIFA imependekeza kuwa kombe la dunia 2022 lichezwe kati ya Novemba na Januari. Picha ya juu ni mchoro wa uwanja wa Al Gharafa ambapo unapendekezwa na wenyeji kutumika katika fainali hizo |
Katibu mkuu wa shirikisho la soka duniani FIFA amesema kuwa michuano ya kombe la dunia 2022 nchini Qatar halitafanyika tena mwezi June au July.
Jerome
Valcke, ambaye alipewa kazi ya kutafuta tarehe mbadala ya kufanyika kwa fainali hizo kutokana na kuaminika kuwa katika cha miezi hiyo hali ya juu joto huwa ni kali kupindukia nchini Qatar, amesema kuna uwezekanao wa fainali hizo zikachezwa kati Novemba 15 na Januari 15.
Valcke
ameiambia redio France Info ya nchini Ufaransa kuwa 'haitakuwa tena mwezi June au July.
Ki ukweli nadhani itakuwa ni kati ya Novemba 15 na Januari 15 angalau.
No comments:
Post a Comment