KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, January 8, 2014

Charles Bonface Mkwasa na Juma Pondamali kuionoa Yanga kambini Antalya Uturuki kuanzia kesho

Picha za mwezi Januari 2013 Yanga ilipofanya ziara kwa mara ya kwanza nchini humo kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ambapo walifanikiwa kutwaa ubingwa wakitokea huko chini ya Ernie Brandts safari hii itakuwa chini ya Mkwasa na Pondamali
Msafara wa watu 33 wakiwemo wachezaji 27 unatarajia kuondoka usiku wa leo kuelekea nchini Uturuki kwa shirika la ndege la Uturki (Turkish Airlines) kuweka kambi ya mafunzo kwa muda wa takribani wiki mbili kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom pamoja na mashindano ya kimataifa.

Kikosi cha Young Africans kitafikia katika Hoteli ya kitalii Sueno Beach Side iliyopo km 70 kutoka katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Antalya ikiwa katika eneo la ufukwe na mji wa kihistoria Magnavat.

Hii inakua ni mara ya pili mfululizo kwa timu ya Young Africans kwenda kuweka kambi katika jiji la Antalya ambapo msimu uliopita pia iliweza kuweka kambi katika mji huo, kambi ambayo ilikuwa na mafanikio makubwa baada ya kurejea nchini kwani timu iliweza kucheza mzunguko wa pili pasipo kupoteza mchezo hata mmoja mpaka ilipotwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Timu itaondoka chini ya kocha msaidizi Charles Boniface Mkwasa na kocha wa makipa Juma Pondamali amabao wataendelea na mafunzo nchini Uturuki wakati uongozi unaendelea na mchakato wa kumpata kocha mkuu ambaye ataungana na kikosi hicho.

Mkuu wa msafara atakua ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salim Rupia ambaye ataongozana na msafara huo kwa kipindi chote cha wiki mbili mpaka kikosi kitakaporejea nchini Januari 23 mwaka huu tayari kwa mzunguko wa pili. 

Msafara kamili ni kama ifuatavyo:
1. Salim Rupia - Mkuu wa Msafara
2. Baraka Kizuguto - Afisa Habari
3. Charles Mkwasa - Kocha msaidizi
4. Juma Pondamali - Kocha wa Makipa
5. Dr. Suphian Juma - Daktari wa timu
6. Hafidh Salehe - Meneja wa timu

Walinda Mlango : Juma Kaseja, Ally Mustafa "Barthez" na Deogratias Munish "Dida"
Walinzi: Mbuyu Twite, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub "Cannavaro", Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Ibrahim Job na Rajab Zahir
Viungo: Frank Domayo, Hasssan Dilunga, Haruna Niyonzima, Nizar Kahlfani, Hamis Thabit na Bakari Msoud
Washambuliaji: Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza, Emmanuel Okwi, Hussein Javu, Said Bahanuzi, Jerson Tegete, Mrisho Ngasa, Saimon Msuva, Shaban Kondo na Reliants Lusajo



Hii ilikuwa ni taarifa ya kocha Ernie Brandts baada ya ziara yao mwezi Januari nchini Uturuki

Walicheza Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawaisha bao dakika za lala salama huku mwamuzi aklishindwa kutoa maamuzi sawa na mshika kibendera wake, ambapo mfungaji alikua maeotea.
 
Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini umakini wa washambuliaji ulitukosesha ushindi kwani Tegete alitumia nafasi aliyoipta kufunga bao la mapema kabla ya Waturuki hawajasawazisha kwa bao la utata  kisha kupewa penati ya utata pia.
 
Mchezo wa mwisho dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza tuliutawala mchezo na kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini wa washambuliaji wetu pia kulichangia sisi kukosa ushindi, kabla ya kipindi cha pili Emmen FC kucharuka na kupata mabo mawili ya haraka haraka kutokana na uzembe wa walinzi na mlinda mlango Yusuph abDUL
 
Tunaushukuru uongozi kwa kukubali kutupa nafasi ya kuweka kambi Uturuki, tumkeaa pamoja kwa mda mrefu huku tukitoka mafunzo kwa vitendo, vifaa na mahitaji yote vikiwepo ,kukiwa na hali ya utulivu, kifupi tumejifunza mambomengi sana ya msingi ambayo yatatusaidia kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom na mashindano yatakayotukabili alisema 'Brandts'

No comments:

Post a Comment