Alvaro Morata amedokeza kuwa kuna uwezekano wa kueleka Arsenal wakati huu ambao anasubiria majaliwa yake ya baadaye ndani ya klabu yake ya Real Madrid.
Bosi wa Gunners Arsene Wenger ameshakata tamaa ya kumpata Morata mwenye umri wa miaka 21 kwa mkopo mwezi huu kuongeza ushambuliaji katika kikosi chake.
Licha ya kutoa ofa ya mkopo ya pauni milioni mbili, Madrid imekataa kumtoa mshambuliaji huyo licha ya kwamba hafikiriwi kuwemo katika kikosi cha kwanza.
Akiongelea juu ya hatma yake ya baadaye mapema wiki hii, Morata amesema inaliangalia wazo la kuondoka Real kama atakosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza.
Arsenal inaaminika kuwa ndio timu pekee kuikabili Real juu ya mpango wa kumchukua, huku pia Tottenham na Liverpool zikitazamwa kwa mbali kama ni wenye nia ya kumchukua mshambuliaji huyo.
No comments:
Post a Comment