KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 15, 2013

MICHAEL RICHARD WAMBURA AJIRIPUA TENA KWA KUCHUKUA FOMU YA UMAKAMU WA RAIS TFF AMPONGEZA TENGA KWA KUTOGOMBEA TENA. NINI MTAZAMO WAKE HUYU HAPA.

Michael Richard Wambura mara baada ya kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais .
Michael Wambura akiongea na waandishi wa habari.
Aliyewahi kuwa katibu mkuu wa shirikisho la soka nchini TFF Michael Richard Wambura na baadaye kukutana na vizingiti lukuki kila alipokuwa anajitokeza kuwania uongozi wa mpira katika ngazi mbalimbali, hii leo amejitokeza tena kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya makamu wa Rais wa shirikisho hilo.

Akionekana ni mwenye matumaini makubwa mara hii na maamuzi yake hayo, Wambura amesema kwasasa amekamilisha jukumu la kwanza la kuchukua fomu kama raia mwenye haki ya kufanya hivyo na kwamba mikakati ya kuelekea katika mchakato mzima wa uchaguzi kwa upande wake ndio unaanzia hapo. 

Amesema angependelea zaidi watanzania zaidi wangejitokeza kuchukua fomu ili kuleta changamoto kubwa zaidi katika mchakato mzima wa uchaguzi huo.

Amempongeza Rais wa sasa Leodigar Tenga kwa kuamua kuachia nafasi hiyo na kwamba hiyo inaonyesha ni namna gani Rais Tenga alivyo muumini mzuri wa vipindi na kuruhusu mawazo mapya na mfumo mpya na watu wapya ili kumpokea nafasi yake.

Amesema unapokuwa madarakani yapo ambayo utayafanikisha na mengine mazuri watu wayaenzi na yale aliyoshindwa wengine watayapokea kuanzia hapo na kuyaendeleza.

Amesema sababu ambazo zimemfanya kuchukua fomu hii leo siyo za wakati ule na kwamba kila jambo linawakati wake na pengine sababu ambazo zilikuwa zikionekana ni tatizo kwa wakati ule huenda zisiwe hivyo kwasasa.

Wambura amedokeza sababu zilizo msukuma kuwania nafasi hiyo ya makamu wa Rais kwakuwa ni nafasi ambayo inachangamoto nyingi na kwamba kuna mengi ambayo hayajafanyiwa kazi kwa kuwa nafasi hiyo haijapata mtu muafaka na kwamba wale wanaomaliza muda wao wanahitaji kusaidiwa.

Ameizungumzia pia sifa ya Rais ajaye kuwa anatakiwa kuwa amechaguliwa kwa mujibu wa katiba na kuupenda mpira wa miguu.

Awe ni mwenye kuelewa kuwa mpira wa miguu unatakiwa kuchezwa nchi nzima kwa kuwa ni mchezo unaopendwa na wengi kote nchini, vilevile awe na muda wa kuushughulikia mchezo wa soka na mwenye kiu ya maendeleo ya soka.

Amesema kuna haja ya kubadilisha mfumo wa soka uliopo ili kuwa na mpira ulio bora, timu ya taifa bora na kutoa nafasi kwa walio wengi kuucheza mpira wa miguu.

Wambura aliwahi kugombea nafasi ya mwenyekiti mkoa wa mara lakini alienguliwa kutokana na kamati ya uchaguzi kusema kuwa hakuwa muadilifu kabla ya kutaka kujaribu tena bahati yake katika chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam DRFA ambapo baadaye aliamua kujitoa na kuelekea katika kamati ya rufaa inayoongozwa na Profesa Mgongo Fimbo ambayo ilimsafisha.

Hata hivyo TFF ilipinga maamuzi hayo na kuelekea shirikisho la soka duniani fifa kuomba mwongozo ambapo FIFA ambalo liliagiza TFF kuunda kamati ya rufaa inayojitegemea ambapo kwasasa mabadiliko hayo yamefanyika.

Kwasasa Wambura yuko safi baada ya maamuzi ya kamati ya rufaa ya Prof Mgongo Fimbo.

1 comment:

  1. Michael Richard Wambura hafai kuwa kushika nafasi yoyote ya soka TFF, alishaipata nafasi hiyo na wadau wa soka tunakumbuka jinsi alivyochangia kwa kiasi kikubwa kizorotesha maendeleo ya soka Tanzania. Itakuwa ni makosa makubwa kumchagua kuwa kiongozi wa soka kwa sasa. Hali ya soka kwa sasa nchini Tanzania imebadilika ukilinganisha na wakati wa utawala wake. Ni vema akawaachie wapenda soka wengine waonyeshe uwezo wao badala ya kumleta mtu ambaye tumeshaona uwezo wake. Katika kipindi chake soka la Tanzania lilitawaliwa na migogoro mingi na hakukuwa na nafasi ya maendeleo ya soka, hatutaki kurudi katika enzi hizo. Watanzania watajuta wakimchagua Wambura kuwa kiongozi wa tena Tanzania

    ReplyDelete