KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 15, 2013

MANCHESTER UNITED YAPATA UDHAMINI WA MAKAMPUNI MAWILI NCHINI CHINA.



 Manchester United imetangaza kupata udhamni wa makampuni mawili ya kichina kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mashetani hao wekundu wanaokadiriwa kuwa na takribani mashabiki milioni 108 nchini China, wametangza kupata udhamini kutoka katika kampuni moja inayotengeneza vinywaji baridi ya Wahaha na benki moja maarufu ya ujenzi nchini China (CCB).
Wahaha wamekuwa wazalishaji wakubwa wa vinywaji nchini Chini kwa miaka 11 ni vinywaji vyao vitakuwa ndio vinywaji marafiki nambari moja nchini humo.
Wamekuwa wakizalisha aina mbalimbali ya vinywaji ikiwa ni pamoja maziwa ambayo yalizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1987 na Zong Qinghou.
Kwa upande wa benki ya CCB ina maana ya kwamba United itapata haki ya kutengeneza kadi zao ambazo zitakuwa na nembo ya klabu katika nchi ya China, na kuwapa faida mashabiki wao 102 ambao wataanza kutumia benki hiyo.

No comments:

Post a Comment