KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 15, 2013

UJUMBE SEATTLE SOUNDERS WAMALIZA ZIARA YAO YA KITALII NA MICHEZO NCHINI . WAFANYA SEMINA KWA WANDISHI WA HABARI JUU YA MAENDELEO YA SOKA NA KUKUTANA NA RAIS TENGA NEW AFRIKA HOTEL.

Rais wa shirikisho la soka nchini Leodigar Tenga  katikati  pamoja na mlinzi wa Seattle Sounders Marc Burch kushoto, Kasey Keller mlinda mlango wa zamani wa kimataifa wa Marekani na vilabu mbalimbali barani Ulaya na Marekani wa pili kutoka kulia ni Kevin Griffing ambaye ni mkuu wa maendeleao na masoko na mashabiki wa klabu hiyo na mwanahabari wao.
Kasey Keller akitoa ujumbe kwa waandishi wa habari wakati wa semina hiyo.
Rais wa TFF Leodigar Tenga akisalimiana na nyota wa zamani wa soka nchini Marekani na Ulaya Kasey Keller na nyuma yake ni mlinzi wa sasa wa Seattle Marc Burch.
Hapa wakionyesha picha ambayo inawakilisha moja ya kivutio cha utalii hapa nchini ikiwa ni eneo muhimu ambalo Seattle Sounders imekuwa ikiwakilisha vema nchini Marekani na kuvutia watalii wengi kuja nchini. Kumbuka serikali ya Tanzania kupitia bodi ya utalii nchini TTB iliingia mkataba na klabu hiyo kubwa nchini Marekani kutangaza vivutio vya kitalii nchini na hiyo imekuwa ikifanyika kupitia uwanja wa soka wa klabu hiyo.

Rais wa TFF Leordigar Tenga akielezea umuhimu wa kuwa urafiki na klabu kubwa katika nchi kubwa kama Marekani katika maendeleo ya soka nchini. Pia Tenga ameelezea juu ya umuhimu wa kuwepo na ongezeko la udhamini katika mpira wa miguu akichukulia mfano wa klabu ya Seattle Sounders ilivyopiga hatua kubwa.
Mkurugenzi wa masoko wa bodi ya utalii nchini TTB Geofrey Meena akizungumzia jambo linalo husu fursa mbalimbali za kiutalii nchini ambazo klabu ya Seattle Sounders imekuwa ikizitangaza kupitia uwanja wa mpira. Pia meena ametanabaisha kuwa kupitia klabu hiyo Marekani imekua ni pili kwa kuingiza watalii wengi nchini Tanzania. Tazama picha ya projector utaona vivutio vya Tanzania vikitangazwa ndani ya uwanjani wa Seattle.
Kutoka kushoto ni Cristine Adding kutoka taasisi ya Washington global hearth allience (WGHA)ambaye naye amefuatana na ujumbe huo katika ziara ya hapa nchini, Kasey Keller, Geofrey Meena, Geofrey Tengeneza ambaye ni afisa uhusiano wa TTB na Kevin Griffing.

No comments:

Post a Comment