KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, January 15, 2013

MAFUNZO YA YANGA UTURUKI KUONYESHWA JUMAMOSI TAIFA KWA BLACK LEOPARD YA AFRIKA KUSINI. ERNEST BRANDTS ANASEMA LICHA YA KUTOKUSHINDA UTURUKI LAKINI TIMU IMEKWIVA


Kocha wa Ernest Brandts amesema licha ya kwamba timu yake ilishindwa kupata ushindi katika ziara yake ya mafunzo ya wiki mbili nchini Uturuki lakini ameridhika na namna vijana wake walivyoyapokea mafundisho yake na sasa vijana hao wamekwiva kwa changamoto ya ligi kuu ya soka Tanzania bara duru la lipi.

Brandts ameshukuru uongozi kwa kuweza kuwapa nafasi ya kufanya kambi ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Taznania bara kwani uwepo wao Uturuki kwa pamoja wamepata nafasi ya kuiunganisha timu kwa pamoja.
Amesema katika michezo miwili ya mwisho vijana wake walionyesha kuiva vizuri na kwamba amepata muda mzuri wa kukaa na vijana wake na wote wameonyesha kuiva kimazoezi.

Amesema mazingira ya kambi yalikuwa mazuri na huduma nyingine pia zilikuwa nzuri na kwamba malengo yake yametimia.

Amerejea kauli yake aliyotoa kabla ya kuondoka Antalya juu  ya michezo mitatu ya kirafiki aliyopata dhidi ya Armini Bielefeld, Deinizlispor na Emmen FC kwa kusema michezo ilikuwa ni mizuri na wamepata nafasi ya kuona mapungufu machache yaliyojitokeza na anaamini watayafanyia kazi na kuendelea kufanya vizuri.
 Tumecheza michezo mitatu, wa kwanza tulitoka sare na Amrinia Bielefeleld, mchezo ulikua mzuri na timu yangu ilicheza vizuri kwa dakika 90 zote za  mchezo licha ya Arminia kusawazisha bao dakika za lala salama.
 Mchezo wa pili dhidi ya Denizlispor nao pia timu ilicheza vizuri na kuweza kutengeneza nafasi nyingi za kufunga licha ya kwamba walipoteza mchezo huo.
kuhusu mchezo wa mwisho Brandts amesifu zaidi kuwa kikosi kilionyesha kandanda la hali ya juu dhidi ya Emmen FC ulikuwa mzuri pia na kwa dakika 45 za kipindi cha kwanza kwamba walitawala mchezo na kupata kupata nafasi kadhaa za kufunga mabao lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake pia kulichangia kukosa ushindi.
 Mara baada ya kurejea kutoka Antalya Yanga inajipanga kwa mchezo wa kirafiki utakao fanyika jumamosi katika uwanja wa taifa dhidi ya timu ya 
 Black Leopard ya Afrika Kusini ambayo inashiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment