Mohamed Samata wa Afrikan Lyon akiwakaribiza wachezaji wa Keller na Marc Burch katika shule aliyosoma yeye na mdogo wake Mbwana. |
Wanafunzi wa shule ya msingi MbagalaMchikichini. |
Wanafunzi wa shule ya msingi Mchikichini wakimsiliza Rahim Zamunda akiwapa maelekezo. |
Mlinda mlango Kasey Keller akivaa buti kabla ya kuanza kucheza soka na wanafunzi wa Mchikichini. |
Marc Burch mlinzi wa Seattle Sounders akifurahia Klinic na wanafunzi wa Mchikichini. |
Rahim naye kumbe wamo. |
Kasey Keller na Marc Burch wakiwa na Mohamed Samata katika picha ya pamoja na wanafunzi. |
JIONI WAKIWA UWANJA WA KARUME.
Huu ulikuwa ni mchezo wa Afrikan Lyon B dhidi ya Simba B ambao ulihudhuriwa na Keller na Burch uiimalizika kwa suluhu ya 0-0 uwanja wa Karume. |
Keller amekuwa
mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Marekani mara nne katika fainali
za kombe la dunia na mmoja wa walinda mlango wa kwanza kuwa namba moja katika
vilabu vya ligi kuu ya nchini England.
Katika miaka
ya 1997,1999 na 2005 alitajwa kuwa mwanamichezo bora wa mwaka ikiwa ni nadra
kupata tuzo kama hiyo mara.
Mzaliwa huyo
wa kitongoji cha Olympia, Keller amecheza zaidi ya mechi katika ngazi ya klabu
na timu ya taifa. Amekuwa mlinda mlango mwenye rekodi kubwa zaidi ya kuidakia
timu ya taifa ya Marekani akidaka michezo 102 na kushinda michezo 53 kati ya
hiyo.
Ameshiriki
kombe la dunia mara nne, ambapo mwaka 1996 alikuwa nahodha wa timu ya taifa ya
nchi hiyo iliyoshiriki michezo ya Olympic.
Alijiunga na
Millwall ya England na kuanza kucheza soka la kulipwa la kueleweka kwa mara ya
kwanza katika ligi ya daraja la kwanza hiyo ilikuwa May 2, 1992 kabla ya
kuelekea Leicester City miaka minne baadaye wakati huo ikishiriki ligi kuu ya
England ‘Premier League’ ambapo mwaka 1997 walishinda taji la ‘League Cup’.
Baada ya
misimu mitatu na Leicester City alijiunga na Rayo Vallecano iliyokuwa
ikishiriki ligi kuu ya Hispania ‘La Liga’. Baadaye alirejea Premier League ambapo
alijunga na Tottenham Hotspur katika misimu miwili ya 2002-03 na 2003-04.
January 15,
2005, Keller alijiunga na Borussia Mönchengladbach ya Ujerumani kabla kuondoka
huko na kurejea kwa mara ya tatu Premier League ambapo alijiunga na klabu ya
jijini London katika viunga vya Craven Cotage na Fulham.
Kwa upande
wake Marc Burch mzaliwa wa Cincinati, Ohio hana historia ya kutisha ambapo
alianzia soka chuo kikuu cha Maryland kabla ya kuelekea D.C. United mwaka 2007
mpaka 2011 na baadaye akajiunga na L.A. Galaxy mwaka 2006 kabla ya kuelekea Columbus
Crew na baadaye mwaka jana akajiunga Seattle Sounders ambayo anaichezea mpaka
sasa.
Huo ndio
ugeni wa kisoka ulioko hapa nchini.
No comments:
Post a Comment