KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, August 14, 2014

Madalali wa Korti wakamata basi la TFF kisa deni la milioni 140


Basi la Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limekamatwa na madalali kwa amri ya mahakama kutokana na deni la sh milioni 140 ambazo TFF inapaswa kulipa kabla ya kurejeshewa basi hilo.
Amri hiyo imetokana na deni hilo la kampuni ya Punchline ya Kenya iliyokuwa ikichapa tiketi za kuingilia uwanjani kuanzia mwaka 2007.

Mpaka kukumatwa kwa basi hilo ni kwamba TFF ilikuwa imekwisha kulipa sh. milioni 70 katika deni hilo.
Taarifa ya afisa habari na mawasiliano wa TFF Bonface Wambura imesema kuwa TFF inafanya Jitihada kumaliza deni hilo. Pia wanachunguza  mwenendo mzima uliosababisha kuwepo deni hilo.

Tukio kama hilo liliwahi kutokea mwaka jana kama picha ya chini inavyoonekana 
Pichani juu ni picha iliyopigwa mwaka jana ambapo kutokana na deni la malimbikizo ya malipo ya makazi ya waamuzi katika hoteli ya SAFINA waliochezesha michuano ya Chalenji mwaka 2011, ilipelekea basi dogo la shirikisho la soka nchini TFF walilopewa na NMB kufungwa mnyororo ndani viunga vya uwanja wa kumbukumbu ya Karume ambapo deni hilo lilifikia zaidi ya shilingi milioni 51.
 
Breakdown ya kampuni ya Flamingo Auction Mart linatekeleza amri ya mahakama ya Kivukoni Kinondoni ya kukamtwa kwa mabasi mawili likiwemo moja kubwa lililotolewa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, deni hilo hatimaye lilimalizwa na sasa mahakama ina amrisha kukamatwa kwa basi kubwa kama ilivyo tolewa taarifa na msemaji wa TFF Bonface Wambura.