KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, August 13, 2014

Jamali malinzi ulimfukuza kazi Saad Kawemba kumbe bado anakufaa TFF?

Mkurugenzi wa zamani wa mashindano wa TFF Saad Kawemba
Bosi wa mpira wa Tanzania Jamali malinzi mara tu alipochaguliwa na kuanza kuliongoza shirikisho la soka nchini TFF, miongoni mwa mambo aliyo anza nayo ilikuwa ni pamoja na kuanza kulisafisha shirikisho hilo kwa kuwaondoa watendaji wake wa kazi za kila siku waliokuwa wakifanya kazi chini ya Rais aliyetangulia Sir Leordigar Chila Tenga,

Miongoni mwa maafisa hao ni pamoja na Saad Kawemba aliyekuwa mkurugenzi wa mashindano ambaye hakuna asiyekubali uchapakazi wake na alivyojitoa kuhakikisha ana kamilisha wajibu kwa misingi ya majukumu aliyokabidhiwa

TFF ni taasisi kubwa sana tofauti na watu wengi wanavyo fikiria. Ili kuiendesha kisasa na kwa misingi ya wakubwa wa mpira duniani wanavyotaka ni lazima upate watu wenye uzoefu, ufahamu, uwelewa, na wenye kujitoa muda kwa ajili ya mpira.

Rais Malinzi wakati anaingia ofisini TFF alikuta shirikisho hilo limejipanga vizuri kisafu likiwa watu sahihi ingawaje walikuwepo wachache waliokuwa wanakwamisha maendeleo kwa namna moja ama nyingine, hao sio mahala pake kuwazunguzia hapa, kwa wale waliokuwa muhimu na ambao umuhimu wao unaendelea kuonekana nje na ndani ya shirikisho hilo, ni  muhimu japo inaonekana kama ni ngumu, ni vema ukawarejesha kwa kulisaidia soka la nchi.
Bora ungeomba ushari kwa huyu jamaa kama anavyokunong'oneza hapo juu usingefanya yale
Umuhimu wa Kawemba unaonekana nyakati kama hizi wa usajili ambapo mfumo wa kisasa wa usajili kwa njia ya mtandao yaani (TMS)ulimuhitaji yeye pamoja na upatikanaji wa hati ya uhamisho wa kimataifa (ITC) kwa wachezaji wa kimataifa.

Leo Saad Kawemba TFF inamlipa kwa kufundisha watendaji wa vilabu akiwa nje ya TFF  nini mantiki yake? ni wazi bado ni nyenzo muhimu katika maendeleo ya mpira wa nchi akiwa bado kijana mwenye uwezo na nafasi ya kulitumikia shirikisho la soka la nchi.Huu si ungwana Malinzi na timu yako nzima kutembea kifua mbele na kujisifia umesafisha watendaji wa Tenga na mambo yako yana kwenda, ilhali bado kuna mkwamo na watu wa mpira wanaona wanakusaidia.

Rockersports imemshuhudia Kawemba akiwafundisha watendaji wa vilabu vya ligi daraja la kwanza wiki iliyopita na Jumanne akikamilisa kuwafundisha watendaji wengine wa vilabu vya ligi ya Vodacom namna ya kufanya usajili wa wachezaji kwa mfumo wa komputer (TMS) katika semina uliyoiandaa kwa watendaji wa vilabu, hiyo si sawa.

KItengo cha ufundi cha shirikisho lolote la mpira duniani ndio jiko la mpira wa mpira wa nchi, ukifanya mchezo kwenye kitengo hicho utakwama sana, angalia namna mambo mengi yalivyokwama mpaka Kawemba na baadhi ya watendaji wa zamani walivyo yakwamua.
Ni aibu kwa kipindi kama hiki kutoa semina ya namna ya kusajili wachezaji ikiwa imesalia wiki moja ya kufunga dirisha la usajili, huo ni mkwamo mkubwa sana.
Pichani mshauri wa mambo ya ufundi wa Rais Malinzi Pelegrinius Rutahyuga( kushoto) akiwa na bosi wake na kulia ni afisa habari na mawasiliano wa TFF Bonface Wambura
Wako watu wengi nje ya TFF wana angalia na kutafsiri mabadiliko uliyoyafanya kama kisasi na kukomoana, kutokana na dhana nzima ya mchakato wa uchaguzi uliopita uliokuweka madarakani, kumbuka zile zilikuwa kambi achana na hayo yamepita sasa kusanya nguvu za ndani za nje kufanikisha mpira wa Tanzania.

Nakumbuka ulitangaza msamaha kwa wale wote aliofanya makosa huko nyuma na hata kufungiwa kwa makosa mbalimbali ya kimpira, sijui msamaha wako ulilenga nini na kwanini, ilhali umesafisha watenda kazi wa kweli ndani ya TFF na leo unalamba matapishi yako? Watu kama Kawemba,Sabri na mzee Mshangama huku paswa kuwaondoa TFF rejea maamuzi yako na tafuta washauri wa mpira na sio hao ulio nao sasa.