Release No. 137
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Agosti 13, 2014
TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) halitambui
mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa
wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.
Uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa
uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao tunautambua, na tutaendelea kufanya nao
kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.
Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal
Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi
ya uongozi wala kamati za muda za utendaji. TFF inafanya kazi za kamati za
utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu.
Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa
Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake.
Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika
kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo
husika kwa hatua zaidi.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
TAARIFA YA COASTAL UNION KWA WANAHABARI
UONGOZI
wa Klabu ya Coastal Union umesema kikao cha wanachama kilichoketi mwishoni mwa
wiki iliyopita kilikuwa na agenda kuu mbili ikiwemo kumjadili Mwenyekiti wao
aliyejiuzulu Hemed Aurora pamoja na utendaji wa Makamu Mwenyekiti na sio kumuondoa
madarakani kiongozi huyo kama inavyofikiriwa na wadau wa michezo hapa nchini.
Mkutano huo
wa dharura uliitishwa na wanachama hao kwa mujibu wa katiba ya Coastal Union ibara
22 kifungu namba 4 na 5 uliofanyika kwenye ukumbi wa klabu hiyo
barabara 11 jijini Tanga.
Katika kikao
hicho kilichohudhuriwa na wanachama wapatao 142 kwa pamoja walikubaliana
kujiuzulu kwa Mwenyekiti wa Klabu ya Coastal Union lakini wakisisitiza kuwa
makamu mwenyekiti wa Klabu hiyo Steven Mguto kumdumaza kiutendaji na sio vyengivyo
ikimaanisha kumsimamisha katika utendaji wake wa kazi za kila siku wala
hajafukuzwa katika nafasi yake hiyo.
Ufafanuzi
huu unatokana na taarifa iliyotolewa na
shirikisho la soka nchini TFF ikieleza kuwa uchaguzi uliofanyika ndani ya klabu
ya Coastal Union hivi karibuni ni batili kitendo ambacho sio kweli kama
kulifanyika uchaguzi kwenye mkutano huo bali ni mkutano ambao uligusa agenda
hizo mbili.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Tanga jana,Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar
Assenga alisema wanashangaa kuona shirikishao la soka nchini TFF wanalivalia
njuga suala hilo wakati bado hawajapata miktasari ya mkutano huo ambao
uliitishwa na wanachama.
Assenga alisema
kinachotakiwa kufanyika hapo ni Makamu Mwenyekiti yeye binafasi baada ya kupewa
tuhumu hizo anapaswa kujitetea kwenye kamati ya maadili ya klabu hiyo na sio
shirikisho la soka nchini kwani kufanya hivyo atakuwa amekiuka taratibu
zilizopo kisheria.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment