Kelvin Yondani |
Geofrey Nyange 'Kaburu' |
Hayo
yameelezwa na makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu
alipokuwa akiongea na Rockersports na kusema kuwa katibu wa TFF Angetile Oseah
‘Ngeta’ ni muongo kwani ameamu kuudanganya umma kwa mahaba yake makubwa kwa Yanga huku akijua wazi kuwa anasema uongo.
KABURU
amesema Angetile ameamua kutoa leseni ya Kelvin na kuruhusu mlinzi huyo kuichezea
Yanga kwenye michuano ya Kagame bila kuruhusiwa na kikao chochote cha kamati ya
utendaji kilichoketi kuzungumzia uhalali wa upande upi wenye haki ya kumtumia
mlinzi huyo.
Simba ilipeleka
jina la mlinzi huyo kama ilivyokuwa kwa Yanga kwa ajili ya kumtumia kwenye
michuano ya kombe Kagame lakini TFF iliamua kumruhusu Yondani kuichezea Yanga.
Aidha Kaburu
amesema tayari barua yao imeshawasilishwa kwa Rais Tenga kwa ajili ya kutafuta ukweli
na Simba inaimani kuwa Kelvin Yondani hatatumiwa tena na Yanga katika michezo
inayoendelea ya kombe la Kagame.
hivi kinachowasumbua simba ni nini?mkataba wa simba ni wa kugushi ndio maana umekosewa sababu ya kufanywa haraka haraka na kiujanjajanja, mkataba wa mwaka 2011 unaandaliwa mwaka 2012ili ionekane ulisainiwa 2011 matekeo yake ndio hayo makosa yaliyojitokeza ambayo simba wanadai ni ya kibanadamu.kama ni makosa ya kibinadamu isiwe kwao tu bali na yondani naye ashirikishwe kuyatatua kwani na yeye ni mdau mkuu wa mkataba huo iwapo kweli alisaini.tufike mahali haya mambo ya kugushi yakomeshwe kabisa katika medani ya soka kwani huko nyuma yalishawahi kutugharimu pale nchi yetu ilipoondolewa kwenye fainali za soka la u-17
ReplyDeletena kama mkataba ulisainiwa 23/12/2011 imekuwaje makosa hayo ya kibinadamu yasigundulike hadi julai 2012?wakati wote Rage alipokuwa anapiga kelele kumbe alikuwa hajagundua makosa hayo?sasa kama mkataba wa simba una makosa inakuwaje yondani na yanga wawasubiri wao simba warekebishe makosa yao?viongozi wa simba wawe majasiri kuwaambia ukweli wanachama wao pale wanapokosea badala ya kutaka kuchafua watu wengine.walishafanya hivyo kwenye suala la kago na hadi sasa wanaona aibu kukiri hadharani kwamba walikosea kuwatuhumu watendaji wa TFF.Mbona madega aliwakabili wanachama wa yanga na kuwaambia ukweli alipomuuza ngassa kwa azam,tuache unafiki
ReplyDeleteUnajua viongozi wa simba wote wababaishaji hata kauli wanazotoa wananishangaza, eti suala hili linaweza kuvuruga amani ya nchi, kwani wapenzi wetu wanataka kuvamia ofisi za viongozi wa yanga, hivi akili zenu zipo timamu kweli yaani kwa sababu ya Yondani tu amani ivunjike.
ReplyDeleteMara kaburu anaongea na waandishi wa habari kisha anampigia simu Okwi ili awathibitishie waandishi wa habari, inawezekana hawajui soko la kulipwa nini? kinachoangaliwa ni fedha na si porojo, endeleeni kutudangaya nyinyi viongozi wetu. Jiandaeni tutawang'ao tu