Mwenyekiti wa Simba Ismail Aden Rage |
Hali
mwenyekiti wa simba wa klabu ya simba Ismail Aden Rage imeelezwa kuendelea
vizuri na anatarajiwa kuanza safari ya kurejea nchini usiku huu.
Rage
aliondoka nchini kuelekea India kwa ajili ya matibabu ya mgongo uliokuwa unamsumbua
amefanikiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na kwasasa yuko katika hali nzuri kuweza
kurejea nchini kuitumikia klabu yake ya Simba ,familia yake na wananchi wa
Tabora mjini.
Akiongea na
Rockersports makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba Geofrey Nyange Kaburu amesema
wanatarajia kuwa na mwenyekiti wao hapo kesho endapo mungu atamfikisha nyumbani
salama.
“ripoti ya
daktari inaonyesha kuwa mwenyekiti wetu amepata nafuu baada ya upasuaji mdogo
aliofanyiwa na anaanza safari ya kurejea nyumba usiku huu”
No comments:
Post a Comment