Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga ameipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao
2-1 ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe
la Shirikisho.
Mechi hiyo dhidi ya Barrack Young
Controllers II ilichezwa jijini Monrovia, matokeo ambayo yanaweka Azam katika
nafasi nzuri ya kusonga mbele baada ya mchezo wa marudiano utakaofanyika
wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Amesema Azam imefanya jambo kubwa, kwani
kushinda ugenini hasa katika nchi za Afrika Magharibi si jambo dogo, hivyo
Watanzania waendelee kuiunga mkono na anaitakia kila la kheri katika mashindano
hayo.
No comments:
Post a Comment