KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, March 21, 2013

KIMATAIFA: FERDINAND AZUA BALAA KWA WAINGEREZA JUU YA KUJITOA KIKOSINI NA KUINGIA GHAFLA KAZI YA UTANGAZAJI


You're having a laugh: Rio Ferdinand trains on his last visit to the Aspire Academy in Doha
Rio Ferdinand amejitetea juu tuhuma nzito dhidi yake baada ya kuamua kujitoa katika kikosi cha timu ya taifa ya England na baadaye kupanda ndege na kuelekea mashariki ya kati kwa lengo kuwa mtangazaji mchambuzi katika kituo cha televisheni cha Aljazeera katika mchezo wa timu ya taifa ya England dhidi ya San Marino.
Taarifa zinaarifu kuwa mlinzi huyo wa mashetani wekundu Manchester United atakuwa akielekea Qatar ufanya kazi hiyo ijumaa ya kesho katika mchezo huo wa kuwani kufuzu fainali za kombe la dunia.
 Ferdinand alijitoa katika kikosi cha timu ya taifa cha England kwa madai ya kusumbuliwa na maumivu ya mgongo yanayomsumbua mara kwa mara lakini baadaye akiwa na mapngo wa kuelekea huko huko kwa kazi ya uchambuzi.
You're having a laugh: Rio Ferdinand trains on his last visit to the Aspire Academy in Doha
Rio Ferdinand akionekana akiwa mazoezini katika kituo cha mazoezi cha Aspire Academy mjini Doha mwezi Januari wakati Manchester United ilipotembelea huko.

Mlinzi huyo wa Manchester United amekubali kuwa mchambuzi wa kituo cha TV cha Al Jazeera katika mchezo dhidi ya San Marino.
Anatarajiwa kufikia na kufanya mazoezi katika kituo cha maraha cha Aspire Academy mjini Doha, ambacho ni kituo kinachopendwa sana klabu yake ya United wakati wa mapumziko ya majira ya baridi.
 Mwezi Januari vinara hao wa ligi kuu ya nchini England walikuwepo katika kituo hicho.
Alipotua Qatar, Ferdinand aliandika kupita ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twita kuwa
'Gonna check into Aspire, state of the art facilities. Nice!'
Luxury: Ferdinand will stay at the Grand Heritage hotel at the Aspire Academy in Doha, QatarFerdinand amefikia hapa Grand Heritage hotel kituo cha  Aspire Academy mjini Doha, Qatar

State of the art: An aerial view of the Aspire Academy that is used by a number of the world's leading football clubs
Muonekanao wa kutoka juu wa kituo cha michezo cha Aspire Academy ambacho vilabu vingi vikubwa hupenda kukitembelea.

Favourite: Ferdinand is a big fan of the Aspire Academy in Doha
Favourite: Ferdinand is a big fan of the Aspire Academy in Doha
Mkuu wa kitengo cha michezo cha televisheni ya Al Jazeera Duncan Walkinshaw amekaririwa akisema 
 ‘Ttulizungumza na Rio juu ya ujio wake hapa Qatar zaidi ya miaka miwili huko nyuma ambapo sasa tunaona mambo yamekaa vizuri'
Ferdinand ni miongoni tu mwa majina makubwa ambayo yamekuwa yakifanya kazi hiyo ya uchambuzi katika vituo mbalimbali vya televisheni vya kiarabu. 
 
Rio Ferdinand ametetea maamuzi ya kuelekea Qatar kufanya kazi ya uchambuzi wa mchezo baina ya England dhidi ya San Marino.
Mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 34 alikuwa akikumbwa na matatizo ya kuwa majeruhi mwaka uliopita kiasi kupelekea kuondolewa mara mbili katika kikosi cha timu ya taifa England kilichocheza michezo miwili ya kuwania kufuzu kombe la dunia.
Amekaririwa mlinzi huyo akikiri kuwa kilichomfanya ajiondoe katika kikosi cha timu ya taifa ni ratiba ya kipindi hicho ambayo aliipanga tangu awali.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa twitter amenukuliwa akiandika
"hakuna tofauti na kile nilicho kifanya siku 10 zilizopita wakati wa mapumziko ya siku 10.............ahsanteni washikaji ".
Ferdinand ambaye ameitumikia timu ya taifa jumla ya michezo 81 amejikuta akipokea malalamiko na ukosoaji mkubwa kufuatia maamuzi yake ya kuelekea Doha kwa ajili ya kuwa sehemu ya watangazaji wa kituo cha TV cha Al Jazeera watakaokuwa wakiutangza mchezo huo.
Mara ya mwisho kwa Ferdinand kuichezea timu ya taifa ya England ilikuwa ni June 2011, ambapo meneja Roy Hodgson alinukuliwa akimtoa kikosini Ferdinand kwasababu za kisoka.
Hata hivyo wiki iliyopita alitajwa tena na Hodgson kujiunga na kikosi cha timu ya Taifa kwa ajili ya michezo miwili ya kuwania kufuzu fainali ya kombe la dunia dhidi ya San Marino na Montenegro.
Liverpool '100% kumbakisha tena Luis Suarez Anfield msimu ujao.
 Mkurugenzi mtendaji wa Liverpool Ian Ayre amesema klabu yake bila shaka itaendelea kusalia na mshambuliaji wake Luis Suarez msimu ujao katika viunga vya Anfield.
Mshambuliaji huyo mwenye umri miaka 26 alikuwa akihusishwa na kutaka kuihama klabu hiyo, endapo itatokea timu itakayo kuwa imepata nafasi ya kushiriki michuano ya vilabu bingwa barani Ulaya itakayo onyesha nia ya kumtaka.

Hata hivyo Ayre alipoulizwa kama ana asilimia mia moja ya kumbakisha mshambuliaji huyo alijibu kuwa anauhakika na hilo.

Suarez alijiunga na Liverpool akitokea Ajax kwa uhamisho uliogharimu pauni milioni 22.7 January mwaka 2011 ambapo msimu huu amefanikiwa kuifungia timu yake ya Liverpool jumla ya mabao 29.

Hata hivyo Suarez hajafanikiwa kucheza michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya wakati huu ambapo kampeni ya Liverpool ya kupata nafasi ya kushiriki michuano hiyo inaonekana kwenda mrama.




 LUIS NANI NA ALEX FERGUSON KUJUA ADHABU ZAO LEO.
 Man Utd's Sir Alex Ferguson and Nani await Uefa decision
Bosi wa Manchester United Sir Alex Ferguson na winga wake Luis Nani hii leo wanasubiri kujua ni adhabu gani itawakumba kutoka shirikisho la soka barani Ulaya ‘Uefa’, kufuatia mchezo wa mwisho wa ligi ya mabingwa Ulaya ambao United walitolewa na Madrid katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Nani huenda akaadhibiwa kusimama mchezo mmoja baadaya kuonyenshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumuingia vibaya Alvaro Arbeloa wa Madrid lakini pia huenda akapewa adhabu ya kusimama kwa muda mrefu.
Sir Alex Furguson anakabiliwa na adhabu itakayo tokana na kutokuhudhuria mkutano na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, kosa ambalo huenda likamgharimu kusimama kukalia benchi la ufundi kwa michezo kadhaa.
Ferguson alikasirishwa na maamuzi ya mwamuzi raia wa Uturuki Cuneyt Cakir ambaye alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Luis Nani hali ambayo imetafsiriwa na meneja huyo kuwa iliwatengenezea mazingira ya ushindi Real Madrid.
Kabla ya tukio hilo la kadi nyekundu, United ilikuwa ikiongoza kwa bao 1-0, kabla ya Madrid kusawazisha baadaye na kuandika bao la pili na hatimaye kutinga robo fainali ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment