KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Thursday, December 22, 2011

Nyota wa Cameroon Samuel Eto'o ameliweka suala lake kuwa zaidi ya mgomo

Nahodha wa Cameroon Samuel Eto'o amesema kamwe hajutiii kile alichokifanya kuhusu mgomo wa kutokuitumikia timu ya taifa ambao umelekea kupewa adhabu ya kutokuitumikia timu ya taifa kwa michezo 15.

Adhabu hiyo imetolewa na shirikisho la kandanda la ncini Cameroon (Fecafoot) kufuatia kugomea safari ya kuelekea nchini Algeria kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa baada ya posho za wachezaji wa timu hiyo kucheleweshewa posho zao.

Anakaririwa Eto’o na moja ya kituo cha luninga cha nchini Cameroon akisema

"hatujutii kitendo chetu tulichokifanya kubwa zaidi tulitaka kuweka mambo wazi na mambo hayawezi kwenda kama ilivyokuwa hapo kabla ".

"tulikuwa tunatumia fursa hiyo kujaribu kutafuta suluhisho katika soka la Cameroon."

Eto'o hajapinga adhabu aliyopewa ya kusimama kuitumikia timu ya taifa kwa michezo hiyo 15 na hivyo atakosekana katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika kwa miaka ya 2013 na kuwania kufuzu mataifa ya Afrika 2014 na kombe la dunia nchini Brazil.

Ameweka wazi kuwa wachezaji hawakuwa na raha kwa kile kinachofanywa na Fecafoot katika mambo mablimbali na mgomo huo haukuwa kwa posho ya kutokezea tu katika michezo hiyo. Anasema namna timu inacyo fanyiwa haiwezi kukubalika.

"ni vigumu kuelezea kwa nini maafisa wanataka walitaka kusafirisha wachezaji kwa masaa manane hiyo kwenda na kufanya mazoezi sehemu nyingine ambapo wakati inawezekana kufanyika hivyo nchini kwetu".

Mashabiki nchini Cameroon wamekuwa wakipanga mipango katika kumpa support lakini Eto'o anasema hakukuwa na haja ya kufanya hivyo na kusisitiza kuwa atarejea katika timu ya taifa lake baada ya kumaliza adhabu yake jambo la msingi ni yeye kusalia katika ubora wake.



No comments:

Post a Comment