KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 2, 2013

MUDA MFUPI UMESALIA KABLA YA KUFUNGWA DIRISHA LA KIANGAZI , JE ? NANI KATI YA ARSENAL NA PSG ATAKAYE PATA SAINI YA MESUT OZIL.

Arsenal ipo katika hatua ya juu kabisa ya mazungumzo ya kutaka kumsajili Mesut Ozil toka katika klabu ya Real Madrid na wanataraji kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Ujerumani kabla ya saa tano kamili usiku wa leo.

Washika mitutu hao wameweka mezani ombi la kiungo huyo kwa mujibu wa chanzo cha habari kutoka nchini Hispania lakini wanakabiliwa na upinzani mkubwa kutoka katika klabu ya Paris St-Germain ambao nao wamepeleka ombi rasmi.

Real Madrid leo imekamilisha usajili leo wa Gareth Bale kutoka katika klabu ya Tottenham kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 86.
Radio moja nchini Hispania 'Cope Radio' imetangaza kuwa Arsenal na PSG wamepeleka ofa mezani kwa ajili ya kiungo huyo wa zamani wa Werder Bremen mwenye umri wa miaka 24.

No comments:

Post a Comment