KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Monday, September 2, 2013

USAIN BOLT AMTAKA DAVID MOYES KUSAJILI VIUNGO WABUNIFU NA HUO NI USHAURI WA BURE BAADA YA KICHAPO CHA LIVERPOOL.

Baada ya kuishuhudia timu yake anayoipenda sana ya Manchester United ikizidiwa kimchezo katika sehemu ya kiungo katika mchezo dhidi ya Liverpool mchezo wa ligi kuu ya England ambao walifungwa bao 1-0, mfalme wa kukimbiza upepo wa mbio fupi Usain Bolt amemtaka meneja mpya wa mashetani wekundu David Moyes kununua viungo wabunifu katika sehemu ya kiungo.

United ilichapwa hiyo jana katika dimba la Anfield ambapo ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi na na kushindwa kumalizia nafasi chache walizopata huku sehemu ya kiungo ambayo ilikuwa ikiongozwa na Michael Carrick, Tom Cleverly na Ryan Giggs ikionekana si lolote si chochote mbele ya Steven Gerrard na Lucas wa Liverpool
.
Bolt raia wa Jamaican, ambaye ni maarufu sana duniani kwa mchezo wa riadha ametupia katika ukurasa wake wa Instagram video yenye ujumbe 
'I'm Usain Bolt and I am a big Manchester United fan. David Moyes, we need a creative midfielder,
One that can pass and create opportunities'

United ina wachezaji kadhaa katika sehemu ya kiungo ambapo wako viungo Shinji Kagawa na Nani lakini bado Moyes anadhani anahitaji kuimarisha kiungo kabla ya usiku wa leo ambapo itakuwa ndio mwisho wa dirisha la usajili.

United ilikuwa katika mpango wa kumsajili Ander Herrera kutoka katika klabu ya Athletic Bilbao kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni £25, ambapo mpango huo ulionekana kupigwa chini na klabu yake Ijumaa.

No comments:

Post a Comment