Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez sasa amethibitisha kuwa anajipanga kukata rufaa juu ya adhabu ya chama cha kandanda nchini uingereza FA kupinga adhabu ya inayomkabili ya kusimama kwa michezo minane baada ya kuthibitika kuwa alitumia lugha ya kibaguzi kwa mlinzi wa pembeni wa Manchester Patrice Evra,kwa mujibu wa mwanasheria wake.
Alejandro Balbi, ambaye ni wakala wa Suarez mchezaji huyo ameshawishiwa "convinced" kuwa adhabu hiyo inaweza kubadilika.
Suarez amesimamishwa kwa michezo minane na kulipa faini ya pauni milioni 40,000 kufuatia kutumia lugha ya matusi ya kibaguzi wa rangi kwa mlinzi Evra.
Akizungumza katika mkutano na wanahabari katika mji mkuu wa Uruguay Montevideo, Balbi amesema shauri hilo la rufaa litatekelezwa na mwanasheria wa Liverpool kwenda FA.
Suarez ambaye amekanusha madai hayo yuko ndani ya siku 14 za kukata rufaa juu ya maamuzi hayo ya adhabu.
FA ilifikia kutoa maamuzi hayo kwa Suarez baada ya kusikiliza shauri hilo kwa siku sita na tuhuma hizo matusi hayo ya kibaguzi kwa Evra yalifanyika katika mchezo uliokwenda kwa matokeo ya sare ya bao 1-1 katika dimba la Anfield October 15.
Chama cha kandanda nchini Uruguayan UFA nacho kimesema kiko tayari kutoa msaada wowote utakao hitajika kwa Suarez na klabu yake ya Liverpool katika rufaa hiyo na Suarez ameshapokea uungwaji mkono toka kwa nahodha wa timu ya taifa ya Uruguay Diego Lugano.
No comments:
Post a Comment