Neymar azomewa na mashabiki wa Brazil
Nyota wa Santos
ya Brazi Neymar amesema hakufurahishwa na namna ambavyo mashabiki walivyo
mchukulia kitabnia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki ambao walipata
ushindi wa bao 1-0 ambapo amewataka mashabiki kuifurahia timu yao badala ya
kumnyooshea kidole mchezaji mmoja mmoja.
Neymar amewakosoa
mashabiki wa taifa lake kwa kukosa uzalendo katika mchezo ambao Brazil maarufu
kama Selecao ilipochomoza na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Afrika kusini mchezo uliopigwa
hapo jana.
Mshambuliaji
wa Zenit St Petersburg Hulk, ambaye ndiye aliyepachika bao hilo tayari huko
nyuma alikwisha wahi kutoa maneno kama hayo ya kuwakosoa mashabiki kuwa kwa
kufanya hivyo wanawavunja moyo wachezaji.
Amenukuliwa
Neymar akisema
"sisi
wote tunajua kuwa hatukuwa katika kiwango kikubwa lakini tumefanikiwa kumepata
ushindi. Nilijisikia vibaya sana kuona mashabiki wakituzomea , sitaki mashabiki
wanipende mimi lakini waiunge mkono timu yao."
Mshambuliaji
huyo wa Santos anadhani tabia ya mashabiki ya kukosoa ndani ya Estadio Cicero
Pompeu de Toledo ilichangiwa na kuwepo makundi ya mashabiki toka katika timu
kubwa hasimu nchini humo.
Ameendelea
kunukuliwa kwa kusema
"sijui
sababu hasa ya kuwepo na tabia hii kwa mashabiki , lakini inawezekana
ikasababishwa na kuwepo na kundi kubwa la mashabiki katika vilabu vya Palmeiras,
Corinthians na Sao Paulo.
"lakini
narudia , wanapaswa kuiunga mkono timu kuliko kuizomea."
Mchezo
unaofuata kwa Brazil ni dhidi ya China ukiwa ni mchezo wa kimataifa wa kiarafiki
jumanne.
Joackim Low akasirishwa na ujerumani kushindwa kutumia nafasi
Meneja wa
timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low amekasirishwa na vijana wake kwa
kushindwa kuzitumia nafasi nyingi walizo pata katika mchezo wa kuwania kupata
nafasi ya kucheza fainali za kombe la dunia licha ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi
ya visiwa vya Faroe .
Mabao mawili
ya Mesut Ozil na lingine la Mario Gotze yameipa Ujrumani points tatu muhimu na
kukalia usukani wa kundi la C.
Amenukuliwa Low
akisema
"ni
wazi tangu mapema tulikuwa na nafasi ya kufunga lakini tatizo letu ni kupoteza
nafasi na si katika mchezo huu pekee"
Mchezo huo
haukuwa mchezo mgumu kwa Ujerumani ambayo baadaye itakutana na Sweden na Austria
katika michezo mingine ya hatua ya makundi kusaka nafasi tya kucheza kombe la
dunia nchini Brazil 2014.
Ameongeza Low akisema
" Faroe
si kipimo kwa Ujerumani kwa timu nyingine tutakazo kutana nazo katika kundi".
Hodgson afurahishwa na Cleverly na
Alex
Meneja wa England
Roy Hodgson amesema amefurahishwa na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Moldova.
Mbali na
hilo amepongeza uwezo wa vijana wake chipukizi katika timu ya taifa Tom
Cleverley na Alex Oxlade-Chamberlain hasa katika mchezo wa jana wa kuwania
kufuzu kucheza fainali ya kombe la dunia dhidi ya Moldova.
Cleverly wa Manchester
United na Oxlade-Chamberlain wa Arsenal wote walikuwa na mchango mkubwa katika
kikosi cha England ambacho kilipata ushindi mkubwa kuwahi kuwata huko nyuma
tangu mwaka 1993 na kumpendezesha meneja wao ambaye amekuwa katika kipindi kigumu
cha kujenga upya kikosi kwa ajili ya fainali ya kombe la dunia 2014 mwaka Brazil.
Hata hivyo
walionekana kufunikwa na mkongwe Frank Lampard, 34, ambaye alifunga magoli
mawili ya mwanzo huku Hodgson akiwataka vijana hao kuongeza juhudi kuwapiku
wakongwe.
Amenukuliwa
Hodgson akisema
"kwa kweli nimefurahishwa sana na Tom na
Alex, imedhirisha sasa kwanini Sir Alex Ferguson anamtumia katika timu yake”.
Mabao
mengine katika mchezo huo yalifungwa na Jermain Defoe kabla ya mapumziko na
mengine yaliwekwa nyavuni na James Milner na Leighton Baines.
Rijkaard: Sijawahi kuona timu nzuri
ya taifa kama Hispania
Kocha wa
timu ya taifa ya Saudi Arabia Frank Rijkaard amepaza sauti na kusema anazimika sana
na timu ya taifa ya Hispania hii ikiwa ni kauli iliyokuja baada ya kuchakazwa
kwa mabao 5-0 hapo jana Friday.
Mabao ya Santi
Cazorla na Pedro yaliwapa uongozi wenyeji kwa mabao 2-0 kabla ya mapumziko na
baadaye Xavi, David Villa na Pedro yakakamilisha idadi ya mabao 5 na ndipo Rijkaard
aliposema anaipongeza Hispania ‘La Roja’ kwa kiwango safi.
Amenukuliwa akisema
"timu
ya taifa ya Hispania inavutia dunia nzima , na sijawahi kuona timu ya taifa
yenye ubora kama Hispania.
"Xavi na
Andres Iniesta ni miongoni mwa wachezaji bora duniani, wanaweza kucheza kwenye
timu yoyote.
"Hispania
ina kila sababu ya kutufunga. Wanatengeneza nafasi . sote tulijua toka mapema
utakuwa ni mchezo mgumu. Tumecheza na timu dunia na hayo ni matokeo sahihi."
Hispania
itaanza kampeni zake za kucheza kombe la dunia jumanne kwa kukutana dhidi ya Georgia.
No comments:
Post a Comment