Kukosekana kwa
kiungo mahiri Michael Bradley na mshambuliaji Landon Donovan mwenye rikodi ya
kihistoria katika soka la Marekani kumepelekea Marekani kupata kipigo cha mabao
2-1 toka kwa wacheza reggae wa Jamaica.
Habari kutoka
katika uwanja wa michezo wa Kingston, Jamaica's Independence Park zimesema
baada ya kuulizwa kocha wa timu hiyo ya taifa wa Marekani Jurgen Klinsmann kwamba
kukosekana kwa Michael Bradley na Landon Donovan ndiyo sababu ya kupokea
kichapo hicho katika mchezo muhimu wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia toka
Reggae Boyz yuko tayari kwa lawama hizo.
Klinsmann amefafanua
kuwa shutuma zote zinapaswa kuelekezwa kwake na kikosi kwa ujumla kwa kuwa
walionyesha mchezo butu usiku wa jana.
"vijana
waliokuwa uwanjani wanastahili lawama kwa kile kilichotokea.
Bradley
amekuwa katika maumivu ya paja aliyo yapata akiwa mazoezini na timu yake ya AS
Roma na tangu mchezo wa kwanza dhidi Catania katika ligi ya Italia Serie A hajashuka dimbani tena
mchezo ambao alitoa pasi za mwisho mbili zilizo pelekea matokeo ya na Catania.
Donovan ni
majeruhi wa msuli tangu mchezo wa kimataifa wa mwezi uliopita dhidi ya Mexico
uliomalizika kwa ushindi wa bao 1-0 uliopigwa katika dimba la Azteca.
Amekaririwa Tim
Howard akisema ,
"tulipata
matokeo mazuri dhidi ya Mexico mwezi uliopita tulipokuwa na wachezaji wazoefu
na hakuna sababu kwa nini tumepoteza mchezo huu"
"Michael
kweli ni mchezaji muhimu kwetu na Landon, kama unavyojua wanafanya mambo ambayo
yanakuwa, lakini sidhani kama hiyo ndiyo sababu, kweli si dhani hivyo. Nafiri tulikosa
umakini katika maeneo fulani"
Klinsmann amesema
katika mchezo huo alikuwa na kikosi cha ushindi katika uwanja ambao jina lake
la utani ni ‘The Office’ uwanja ambao katika historia yake Marekani ilipata sare
mara nne , na sasa wamepoteza.
No comments:
Post a Comment